Baadhi ya maradhi ni kwa ajili ya jinsia fulani tu. Hapa tunazungumzia ugonjwa ambao huwapata wanawake pekee (PID)
Sitaki nikuchoshe;--
ILA
Huenda ukawa ndio mara yako ya kwanza kukutana na jina la ugonjwa huu.
Kama jibu ni 'NDIO', basi wacha nikujuze;-
PID ni kirefu cha neno “Pelvic Inflammatory Disesase’ Ni ugonjwa wa maambukizi unaotokea katika via vya uzazi wa mwanamke ambapo huhusisha maambukizi katika shingo ya kizazi (CERVICITIS), nyama katika mfuko wa uzazi (ENDOMETRITIS) na mirija ya uzazi (SALPINGITIS)
Unajua kwanini nimeamua kukudokezea dondoo hii?
Kwasababu
Kundi kubwa la wanawake wamekuwa wakiteseka na tatizo hili, bila kupata msaada wa tiba huku wakibaki na madhara makubwa kama ugumba n.k.
Unajua kwanini nimeamua kukudokezea dondoo hii?
Kwasababu
Kundi kubwa la wanawake wamekuwa wakiteseka na tatizo hili, bila kupata msaada wa tiba huku wakibaki na madhara makubwa kama ugumba n.k.
VYANZO NA VIHATARISHI VYA KUPATA UGONJWA WA PID
Vimelea aina ya
NEISSERIA GONORRHEA pamoja na CHLAMYDIA TRACHOMATIS ndio chanzo cha maambukizi
ya ugonjwa wa PID ingawaje kuna aina kadhaa za vimelea vinahusishwa kusababisha
ugonjwa wa PID hivyo nilivyotaja ndio vinaongoza Kwa umaarufu kusababisha
ugonjwa huu.
ZIKO NJIA HATARISHI AMBAZO HUSABABISHA MAAMBUKIZI HAYA NAZO
NI;-
- Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa
uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango
- Kufanya ngono isio salama (Ngono zembe)
- Maambukizi katika njia za uzazi baada ya kujifungua ama mimba kuharibika.
- Kuambukizwa kupitia damu iliyo athirika na ugonjwa huu.
- Kupata maambukizi kupitia wakati wa kutoa mimba kwa njia zisizo salama.
DALILI ZAKE
Kuna dalili mbalimbali
zinazoweza kuashiria ugonjwa huu wa PID miongoni mwa dalili hizo ni;-
- Mwanamke kupata maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
- Kupata maumivu wakati wa kukojoa
- Kupata homa na kuhisi kichefuchefu
- Kupata maumivu ya mgongo na kutapika
- Kutokwa na hedhi bila mpangilio
- kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Kutokwa na uchafu mweupe ukeni unaotoa harufu mbaya
NJIA ZA KUEPUKA UGONJWA WA PID
Pamoja na kuwepo kwa
dawa za kutibu tatizo hili ni vyema ukajiepusha na vihatarishi vya kupata tatizo hili kwa
kuzingatia yafuatayo,
- Epuka kufanya
ngono isiyo salama.
- Jiwekee tabia
ya kufanya vipimo mara kwa mara hasa kizazi
- Usifanye mapenzi mara baada ya kujifungua au mimba kutoka mpaka utakapohakikisha shingo ya uzazi imefunga vema.
- Kuwahi kuonana na daktari unapoona dalili za ugonjwa
- Kuwa msafi na
kula lishe bora
Note:
Uonapo dalili za
ugonjwa huu wahi kupata matibabu kwani ugonjwa huu huweza kusababisha
ugumba ikiwa hautapata tiba vizuri.

COMMENTS