Je wajua kuwa kula kupita kiasi kunaweza kusababisha shida katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula..?
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni jumla ya viungo vya mwili vinavyofanya kazi ya kuingiza chakula mwilini, kukisaga, kukisafirisha, na kukimeng'enya.
Kukimeng'enya maana yake ni kuondoa lishe inayohitajika mwilini na kuyatoa mabaki nje ya mwili kwa njia mbali mbali.
Viungo vya mwili vinavyohusika kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni
- Kinywa
- Koo (Umio)
- Mfuko wa tumbo
- Ini
- Mfuko wa nyongo
- utumbo mwembamba
- Kongosho
- Utumbo mpana n.k
SABABU ZA TATIZO LA MMENG'ENYO WA CHAKULA
- Kula kupita kiasi
- Kula hovyo
- Kula chakula haraka haraka
- Kula vyakula vigumu sana
- Kula vyakula ambavyo huchelewa kumeng'enywa. Mfano ni kama nyama nyekundu, vyakula vyenye mafuta mengi ama sukari nyingi
- Kula chakula huku unakunywa maji
DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MFUMO WA MMENG'ENYO
- Kutokupata choo kwa mda mrefu
- Kupata choo kikubwa kwa uchache
- Kutoa haja kubwa ngumu au mfano wa kinyesi cha mbuzi
- Kinyesi kuwa na harufu kali kupita kiasi au rangi nyeusi
HAYA NI BAADHI YA MADHARA YA TATIZO LA MMENG'ENYO
- Kuumwa tumbo mara kwa mara. Hii ni kutokana na uchafu uliojilimbikiza tumboni na kuzalisha bakteria wabaya mwilini.
- Kuumwa kichwa mara kwa mara
- Ngozi kukunjana mithili ya mzee
- Kupata kansa ya tumbo. Hii ni kutokana na kuacha uchafu kuozea ndani
- Kusumbuliwa na magonjwa ya figo na ini
- Kukosa / Kupungua kwa nguvu za kiume
TIBA YA MATATIZO YA MMENG'ENYO
Kwa bahati nzuri tatizo hili limekuwa na tiba za aina tofauti.
A. TIBA YA MAJI
- Kunywa maji mengi (lita tano kwa siku)
- Kunywa maji ya uvuguvugu kila siku asubuhi kwa muda wa siku tano
- Chukua mfuko wa kuwekea maji (water bag) weka maji ya uvuguvugu kisha uweke tumboni kwa muda wa dakika tano.
B. TIBA YA MAZOEZI
- Lala chali, nyanyua miguu yako na kushusha chini mara nyingi
- Mazoezi ya kukimbia
- Mazoezi ya yoga
C. TIBA YA MASAJI (MASSAGE)
- Chukua mafuta ya mzaituni kisha massage (Jichue) katika tumbo
D. TIBA YA VYAKULA NA MATUNDA
- (Siku ya kwanza) Kula machungwa matano asubuhi iwe kifungua kinywa
- (Siku ya pili) Kula ma apple (Japo mawili) yawe kifungua kinywa
- (Siku ya tatu) Kula papai (Liwe kifungua kinywa)
- (Siku ya nne) Kunywa juisi ya limao na asali
- Pia unaweza kutia unga wa mbegu za mlonge katika uji
ASANTE KWA KUWA NASI
Dah somo zuri sana sana
ReplyDeleteUbarikiwe najifunza mengi kwao🔥🔥🔥
ReplyDeleteAsante sana tuko pamoj
DeleteMungu akubariki kwa somo zuri akuongezee ujuzi wa kupambana mambo mengi
ReplyDeleteAaamiin aaamin
DeleteBinafsi Ili tatizo linanisumbua sana Asante kwa elimu hii
ReplyDelete