Maumivu ya kichwa ya kawaida ni tofauti na maumivu ya kipandauso..... Soma makala hii kuelewa vizuri
KIPANDAUSO NI NINI?
Ni maumivu makali ya kichwa ambayo mara nyingi huuma upande mmoja. Yawezakuwa upande wa mbele au upande mwingine wa kichwa. Maumivu haya yanaweza kudumu kwa muda wa kuanzia masaa manne hadi 72.
DALILI ZA KIPANDA USO
Hizi ni baadhi ya dalili za ugonjwa huu ambazo kitaalamu zimegawanyika katika makundi manne (4)
Prodrome, Aura, Headache na Postdrome
1. Prodrome
Hizi ni dalili ambazo hutokea siku kadhaa kabla ya tatizo kutokea. Zinaweza kuwa siku mbili au tatu kabla. Na dalili hizo ni hizi
- Njaa kali kupita kiasi
- Shingo kuwa ngumu (kukakamaa)
- Miyayo mingi isiyozuilika
- Msongo wa mawazo
- Kukosa choo au choo kuwa kigumu
2. Aura
Dalili hizi hutokea kutokana na mabadiliko kwenye mfumo wa fahamu na hudhuru mfumo wa hisia na matokeo yake mtu anaweza kuona mwanga mkali wakati hakuna mwanga, kuhisi mguso n.k
Lakini kundi hili la dalili huweza kujitokeza kabla au baada ya ugonjwa.
Hivyo huweza kusababisha mambo haya
- Kupoteza uwezo wa kuona
- Kuhisi kuchomwachomwa mwilini
- Pia wakati mwingine husababisha ganzi miguuni
3. Headache
- Kichefuchefu na hatimaye kutapika
- Kizunguzungu
- Kupata shida unapokuwa kwenye mwanga
- Kichwa kuuma upande mmoja
4. Pastdrome
Hiki ni kipindi cha mwisho kutokea baada ya kupata kipandauso. Hiki ni kipindi ambacho mgonjw anaweza kuhisi kuwa ameisha au mtupu na wengine huhisi furaha ya uongo.
MAMBO GANI HUCHOCHEA KIPANDAUSO?
Mambo haya yakitokea / kufanywa huchochea ugonjwa huu kwa muhusika hivyo ni vyema kukaa mbali nayo ama kujiepusha.
- VYAKULA
Vyakula vyenye chumvi nyingi, vyakula vilivyochacha huweza kuamsha kipanda uso
Pia kuna baadhi ya vyakula ambavyo huamsha kipanda uso ni kama vile;-
- Vinywaji vyenye caffein kama vile Kahawa
- Vinywaji vyenye sukari isiyo ya asili kama vile Juis cola
- Matunda jamii ya machungwa
- Nyama yenye kemikali ya nitrates
Soma pia
MAMBO MENGINE YANAYOCHOCHEA KIPANDAUSO
- Unywaji wa pombe
- Kulala sana / Kutokulala kabisa / Kidogo
- Harufu kali kama vile udi, pafyumu, petroli n.k
- Uvutaji wa sigara
- Kutofanya mazoezi
- Stress / Msongo wa mawazo
- Kutokunywa maji mengi
- Kunywa mvinyo mwekundu (RED WINE)
- Jeraha la kichwani
TIBA 7 ZA ASILI ZA KUTIBU KIPANDA USO1. CHUMVI
Unaweza kujitibu / kumtibu mtu kipanda uso kwa kutumia chumvi kwa kufanya hivi;-
Andaa maji ya kuoga yamoto. Kisha chukua chumvi (ya mawe itapendeza zaidi) Tia vijiko viwili kisha tumbukiza kichwa au mwili wako wote katika maji yale na utulie kwa muda wa dakika 15.
2. APPLE (TUFAA)
Siku zote kula matunda ni jambo jema, lakini kwa upande wa eppo ni kinga na dawa dhidi ya ugonjwa huu mbali na ladha yake nzuri.
Soma na
Ulaji wa tufaa moja kila siku ni kinga dhidi ya ugonjwa huu, lakini pia unashauriwa wewe ambaye umepatwa na kipandauso unaweza kula tunda moja tu au kunusa maganda yake.
3. CHAI YENYE TANGAWIZI
A. Tengeneza chai ya tangawizi bila kuweka majani ya chai, tangawizi iwe fresh na iwe mbichi kisha kunywa vikombe viwili kwa siku moja. Hii tiba nzuri sana
B. Pia unaweza kutafuta tangawizi mbichi pale ambapo umepata maumivu haya na yatakwisha.
4. UNGA WA MDALASINI
Chukua mdalasini changanya na iliki kisha saga unga wake changanya na mafuta ya ufuta. Mchanganyiko huo utautumia kupaka na kuchua / kumasaji sehemu yenye maumivu. Fanya hivyo kisha wacha kwa muda wa lisaa na baadaye jisafishe.
Fanya tiba hiyo mara moja kwa siku mpaka pale ambapo maumivu yatakapokwisha
5. PILIPILI KICHAA NA LIMAU
Pili pili kicha ni dawa nzuri hata ya maumivu mengine mbali na kipandauso. Chukua pilipili kichaa ikate nusu kisha iweke katika maji (kwenye kikombe). Changanya na maji ya limau au asali kisha koroga na ichanganyike vizuri. Kunywa mara moja kwa siku.
6. KAHAWA NA LIMAU
Ukipata maumivu ya kipandauso, kunywa kikombe cha kahawa ambayo imechanganywa na maji ya limau kijiko kimoja.
Tahadhari!!
Pamoja na kuwa Kahawa ni dawa ya kipandauso lakini unashauriwa usizidishe matumizi yake ya kila siku kwani kaffein iliyomo kwenye kahawa ina madhara mengine kiafya.
Pata na faida hii
7. KIPANDE CHA BARAFU
Hii ndio tiba yamwisho ya asili ambayo nimekuwekea leo katika njia hizi 7.
Chukua kitambaa safi, weka kipande cha barafu ndani kisha pitisha taratibu sehemu yenye maumivu kwa muda wa dakika zisizopungua 10.
Unashauriwa maumivu yanapozidi basi muone daktari.
MADHARA YATOKANAYO NA KIPANDAUSO
- Kifafa
- Kiharusi
- Maumivu sugu ya kichwa
COMMENTS