Furaha yangu ni kukuona wewe ukisoma makala hii. Unaweza kuwasiliana nami kwa namba - 0625 71 80 40
Kwa jina maarufu hujulikana kama Ngogwe. Hivyo tunaweza kusema ni FAIDA ZA KULA NGOGWE / The 7 benefits of African eggplants
Ni kungo muhimu sana ambacho watu wengi hukutumia katika mboga, Lakini ninaimani kuwa ni wachache wanaojua faida zake. Hapa nikutajia faida 7 muhimu ambazo ni lazima uzifahamu kuhusu nyanyan chungu (ngogwe).
1. Huboresha afya ya mwili
Ngogwe ni miongoni mwa mboga zenye virutubisho vingi ikiwemo vitamin A, B na C. Hivyo huboresha afya ya mwili kwa ujumla.
2. Husaidia mzunguko wa damu
Ndani ya nyanya chungu kuna vitamin K inayosaidia kuipa nguvu mishipa ya damu hivyo husaidia zoezi la mzunguko wa damu katika miili yetu.
Mzunguko wa damu unapokuwa mzuri hata baadhi ya kazi zitakwenda vema ikiwemo katika suala la kujamiiana kwa mwanaume.
3. Kuuwa vijidudu mwilini
Kama jina lake lilivyo "Nyanya chungu" na ladha yake pia ni chungu. Na wataalamu wanasema kuwa hii ni sawa na dawa za 'antibiotic' ambayo husaidi kuuwa vijidudu mwilini.
4. Huongeza maji mwilini
Karibu asilimia 90 ya nyanya chungu ni maji, hivyo licha ya kuongeza maji mwilini lakini pia ina madini ya potassiam.
5. Kuimarisha ngozi
Hii ni kutokana na vitamin A vinavyopatikana kwa wingi katika ngogwe. Sambamba na kuimarisha ngozi na kuwa nyororo lakini pia huimarisha uwezo wa macho kuona vizuri.
6. Tumbo kujaa gesi
Nyanya chungu humsaidia mtu kuepukana na matatizo ya tumbo kujaa gesi lakini pia huwasaidia wanaume kuepukana na ugonjwa wa ngiri.
Soma pia Mazoezi 6 yanayo ongeza nguvu za kiume
7. Msaada kwa wenye kisukari
Nyanya chungu ni kiungo ambacho husaidia kupunguza kiwango cha sukari.
Hivyo ni muhimu katika chakula chako kula nyanya chungu japo mara mbili kwa wiki ili kupata faida hizi hapa juu.
Shukrsni
ReplyDeleteGood kijana
ReplyDeleteTuwwkee na faida za kula ndizi au mapapai
ReplyDeleteShukran. Tutaweka inshhaallah
Delete