Kuna sharti moja kubwa kama utalitekeleza basi yaliyobakia yatakuwa madogo na utafanikiwa. Karibu katika makala hii
Asilimia nyingi ya vijana wamepitia / wanapitia katika hatua hii ya kujichua na baadhi yao wanataka kuacha lakini hawajui ni jinsi gani wanaweza kujinasua katika mtego huo.Makala hii itakupa mwanga mpana wa kuweza kuepukana na punyeto na kama ulishaanza kupata madhara basi utarudi katika hali yako kama zamani.
Kuna makala niliandika kuhusiana na mashara ya kujichua. Kama hukubahatika kuisoma basi nimekuwekea hapa.
Madha ya kujichua (punyeto)
Twende sambamba nami
Kuna sharti moja kubwa kama utalitekeleza basi yaliyobakia yatakuwa madogo na utafanikiwa. Shariti lenyewe ni hili
"JE upo tayari kuacha au unajaribu kuacha?"
Hebu jiulize katika nafsi yako kisha jibu bakia nalo.
Endelea na makala;-
1. Acha kuangalia video za ngono:
video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie punyeto. Hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako.
2. Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga:
Bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.
3. Epuka kukaa nyumbani peke yako
Mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine.
4. Fikiria kuhusu madhara yake
Bila shaka madhara umeyasoma hapo juu, kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata hasa madogo madogo kama uchovu mkubwa, kuumwa kichwa na kusahau sana hii itakupa moyo wa kuendelea kutopiga punyeto.
5. Acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho
Acha kuanza sasa hivi. Usiseme ngoja nikapige mara ya mwisho. siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema hivo hivo, kama unaacha acha mara moja.
6. Tafuta mpenzi kama huna kabisa
Ni ngumua kuacha punyeto hali ya kuwa huna mke wala mpenzi.
Ukiwa na mpenzi madhara ya punyeto kama kupungukiwa nguvu za kiume yatakufanya uache kabisa kwani ukiendelea utaaibika siku moja pale uume utakaposhindwa kusimama kabisa mkiwa faragha chumbani na pia utapata nafasi ya kushiriki tendo la ndoa hivyo kuacha kabisa punyeto.
Pia unaweza kumshirkisha mwenzi wako tatizo lako ili akusaidie kuacha.
7. Anza mazoezi na jishughulishe na mambo mengine
Hii itakufanya uwe bize na mambo mengine na utumie mda wako mwingi huko, pia mazoezi ya jioni yatakufanya uchoke na kushindwa kufikiria kupiga punyeto wakati wa kwenda kulala.
Mazoezi kama push up, squarting, kukimbia, kuruka kamba na mengine mengi ni tiba nzuri ya kuacha punyeto.
Tambua kuwa punyeto ni haramu na imekatazwa karibu na dini zote. Hivyo acha kwa kumuogopa Mwenyezimungu kulingana na imani ya dini yako.
9. Dhibiti maongezi yako na mpenz wako aliye mbali
Mara kadhaa kupandishana hisia katika maongezi baina ya wapenzi wawili huchochea katika kujichua.
Jitahidi kujidhibiti pale ambapo unaongea na mwenzi wako aliyembali isifike hatua ukaanza kujichua kwa sababu hiyo.
Jikubali, jiamini jipende. Haiwezekani kijana mzuri kama wewe lakini iwe kuna muda unajifungia ndani halafu unajichua kitu ambacho ni cha aibu kama ukijulikana. Hebu jiulize umekosa nini mpaka ujimalize mwenyewe?
TAFAKARI!!
Soma pia
Kijana acha punyeto, siku moja utaaibika na utajuta
COMMENTS