Ni vema kujua matibabu kabla hujaumwa. Jino ni miongoni mwa magonjwa yanayowasumbua wengi. Njia hizi zitakusaidia kujitibu hata ukiwa nyumbani...
Maumivu ya jino yasikie tu kwa mwenzako, usiombe yakukute. Lakini kama hayajakukuta ni vema ukasoma somo hili ili siku moja unaweza kumsaidia mtu mwingine.
Hapa chini ni tiba 6 za asili ambazo ukichagua moja na kuifuata vizuri basi humaliza kabisa maumivu ya jino / meno yako.
Soma hapa kujua
1. ALOEVERA (MSHUBIRI)
Chukua shubiri safi, katakata kisha kamua utomvu / maji yake na uweke kwenye jino linalouma. Fanya hivyo kutwa mara mbili (asubuhi na jioni)
2. MAJI YA UVUGUVUGU NA CHUMVI
Inaweza kuwa ni fizi au jino, chukua kikombe cha maji ya uvuguvugu weka nusu kijiko cha chumvi. Tumia mchanganyiko huo kupigia mswaki kutwa mara mbili (asubuhi na jioni)
3. PILI PILI NA CHUMVI
Pili pili na chumvi vyote kwa pamoja vina uwezo wa kudhibiti bakteria hivyo mchanganyiko wake waweza kuwa dawa nzuri zaidi. Chukua pili pili manga isage kisha changanya na chumvi ya mawe, weka na maji kupata uji mzito kisha utaweka kwenye jino linalouma kila siku kwa siku kadhaa na maumivu yatakwisha
4. KITUNGUU SWAUMU
Kitunguu swaumu ni miongoni mwa anti biotic za asili tofauti na antibiotic nyingine. Chukua punje mbili za kitunguu swaumu kisha kisage, unaweza kuchanganya na chumvi ya mawe kidogo kisha weka sehemu yenye jino linalouma.
5. MAJANI YA MPERA
Unaweza kutafuna majani kadhaa kila siku, au chemsha majani hayo kisha weka na chumvi kidogo na uwe unapigia mswaki kwa siku mara mbili.
6. ASALI NA MDALASINI
Asali vijiko vitatu, mdalasini kijiko kimoja. Changanya kisha uwe unaweka sehemu yenye jino linalouma kutwa mara tatu
Maumivu yanapoendelea ni vema kumuona mtaalamu wa afya kwa ushauri zaidi.
ANGALIZO!!
Kwakuwa ugonjwa wa meno husababishwa na bakteria ambao wanatokana na mabaki ya vyakula mbali mbali tunavyokula, hivyo ni vema kuzingatia haya yafuatayo;-
- Punguza / acha ulaji wa vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi za viwandani
- Simamia usafi wa kinywa chako vizuri kwa kupiga mswaki walau mara mbili kwa siku.
COMMENTS