Kama hujakutana nalo katia kachumbari basi unaweza ukawa umeshawahi kulitafuna. Hapa fahamu faida zake (TANGO)
Katika kipengele chetu cha afya, leo nakuhabarisha kuhusiana na faida za kula tunda aina ya Tango (cucumber).
Hili ni miongoni mwa matunda ambayo yanapatikana sana katika maeneo yetu. Pamoja na hayo huenda wengi hatufahamu kinachopatikana katika tunda hili lenye rangi ya kijani halisi.
Hizi zifuatazo ni faida chache katika nyingi zinazopatikana.
1. Kuongeza maji mwilini
Hii husaidia hasa kwa wale ambao ni wavivu wa kunywa maji, pendelea kutafuna tunda hili mara kwa mara kwani lina maji mengi.
2. Huongeza vitamin A, B na C
Vitamin hivi huongeza kinga ya mwili na kupata nguvu za kutosha. Unaweza kutengeneza juis ya tango iliyochanganywa na spinach na karoti kisha ukanywa.
3. Kuondoa sumu mwilini
Kwakua tunda hili lina kiwango kikubwa cha maji, hivyo husaidia kuondoa taka mwilini zikiwemo ambazo ni pamoja na sumu mbali mbali.
4. Kupambana na joto mwilini
Unywaji wa juis ya tango pia husaidia kupunguza joto ndani na nje ya mwili (Heart burn). Lakini pia kupaka kwenye ngozi kunaweza kukusaidia kuungua na jua.
Juis ya tango |
5. Husaidia katika urembo
Kutokana na madini ya silica yanayopatikana katika tango husaidia kung'aa kwa kucha na nywele.
Mbali na hayo, yapo pia madini ya silcon ambayo husaidia kuondoa uvimbe kwenye ngozi.
6. Huondoa harufu mbaya mdomoni
Chukua kipande cha tango weka mdomoni kwa angalau dakika 5. Fanya hivi mara tatu kwa siku husaidia tatizo hili. Pia pendelea kutafuna matango mara kwa mara.
Unaweza kupitia na makala hii
7. Kusaidia mmengenyo na kupunguza uzito
Hii ni kutokana na uwepo wa Fibres pamoja na maji mengi hivyo husaidia kuondoa tatizo la kupata choo kigumu na kuufanya mmeng'enyo wa chakula kufanya kazi ipasavyo.
Soma pia
Tatizo la mmeng'enyo wa chakula na tiba zake
8. Kupunguza aina kadhaa za kansa
Hii ni kutokana na virutubisho vinavopatikana katika tango kama vile pinoresinol, secoisolariciresinol na lariciresino Husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa kama vile kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa mwanamke, kansa ya kizazi kwa wanawake pia vile vile kansa ya tezi dume kwa wanaume.
9. Huwasaidia wagonjwa wa kisukari
Tango lina uwezo wa kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu na kuweza kudhibiti shinikizo la damu la aina zote yaani LOW na HIGH blood pressure.
Lakini pia tango lina homoni ambazo zinahitajika kwenye chembechembe za kongosho ili kuweza kutengeneza insulin ambayo huweza kusaidia kudhibiti kiwango cha sukari, hivyo huwasaidia wagonjwa wa kisukari.
UTALIJUAJE TANGO BORA?
- Angalia tango ambalo lina rangi ya kijani iliyo kolea (Dark green)
- Angalia tango ambalo bado ni gumu (halijalegea)
Safi sana
ReplyDeleteAsante kwa kuwa nasi
Deletekwa habarizi na ujuzi kuhusu technology pita hapa kafukuict.blogspot.com
Delete