AGIZO KWA AKINA DADA

     

     

Dada wapendwa wa Kiislamu, mwezi mtukufu wa Ramadhani hutujia mara moja tu kwa mwaka. Tunapokaribia kuumaliza mwezi wa Sha’bani, huwa na furaha tele nyoyoni mwetu ya kuukaribisha mwezi wa Ramadhani. Na kwa wakati huu hatunalo ila kumshukuru Mumba wetu aliyetuongoza kwenye njia yake nyofu (ya Kusilimu), maana lau si Yeye, kamwe hatungeongoka.

Dada wapendwa, tunapaswa kukumbuka kwamba, kufunga siyo kutozingatia kula na kunywa tu na hatimaye kutayarisha futari, bali kufunga kunakotakikana ni kuzingatia maamrisho yake Sub'haanuhu Wata’ala na Mtumewe (s.a.w.).

Miongoni mwa maamrisho yake kwetu ni kuwatii waume zetu kwani Mwenyezi Mungu hako tayari kuzipokea Saumu zetu tukiwa na ufidhuli kwa waume zetu kwani Mola wetu Anatuambia katika Qur'ani: "Waume ndio wasimamizi wa wanawake."

Naye Mtume (s.a.w.) anasema kutufunza namna ya kutunza nyumba zetu kwamba "Mwanamke akifunga Saumu yake ya wajibu, asali sala zake fardhi na amtii mumewe, bila shaka ataingia peponi."
Huo ndio wajibu wetu. Ama mtindo wa kuwasengenya wenzetu, majirani zetu, waume zetu, au waume wa wenzetu ni kinyume cha dini ya Islam, na wakati wowote ule haitakikani kuendesha mikutano ya namna hii, na hasa katika Ramadhani, maana yanaweza kukuharibia Saumu yako.
Pia kujifahiri kubughudhiana, kukaripiana, kunyimana vifaa vya nyumbani kama shoka, chumvi, mwiko n.k. na kujiunga katika makundi ya karata hasa na waume ni dhambi.


Wabillaahi tawfiiiq

COMMENTS

 


 


TANGAZO TANGAZO

TANGAZO  TANGAZO

Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,7,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: AGIZO KWA AKINA DADA
AGIZO KWA AKINA DADA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh8Swc6HP55FyZC9lngT_Ah0FgNjWNabze-9eROpbUHPMXQYiJwtqWNAtqkDoCDey-zXrf_0gmzw-LLwLkT8PkNGri7jpFzkZnpgFzbrFfJss9pfda5xU8JtsJy66hJ3e4vZcIaHR8D7XA/w194-h159/ramadhan_kareem_by_sammiharja.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh8Swc6HP55FyZC9lngT_Ah0FgNjWNabze-9eROpbUHPMXQYiJwtqWNAtqkDoCDey-zXrf_0gmzw-LLwLkT8PkNGri7jpFzkZnpgFzbrFfJss9pfda5xU8JtsJy66hJ3e4vZcIaHR8D7XA/s72-w194-c-h159/ramadhan_kareem_by_sammiharja.jpg
mrbunduki
https://sayyidbunduki.blogspot.com/2018/05/agizo.html
https://sayyidbunduki.blogspot.com/
https://sayyidbunduki.blogspot.com/
https://sayyidbunduki.blogspot.com/2018/05/agizo.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content