Watu wanaamini kila kidonge kinatibu maradhi mbali mbali katika dunia.
Kitu ambacho wengi hatufahamu ni kuwa baadhi ya vidonge ni sumu, hasa kikitumiwa kinyume na maelekezo ya daftari.
Na baadhi ya vidonge huwa tunavitumia bila hata ya maelezo ya daktari.
Vidonge ambavyo mara nyingi huvitumia kienyeji ni pamoja na aina hizi tano ambazo nimekuandalia hapa chini;-
- Antibiotics (Vijiuwa sumu)
- Sleeping pills (Dawa za usingizi)
- Anti infalmmatory (Dawa za kuchua)
- Analegies (Dawa za kupunguza maumivu)
- Steroids (Dawa ya pumu)
*_______________*
Wacha tuone ufafanuzi wa kila moja hapo juu.
1. Antibiotics (Vijiuwa sumu)
Hizi ni aina ya dawa ambazo binadamu wanazitumia katika kutibu magonjwa mbali mbali kama vile kifua, mafua, mafindo findo n.k.
Magonjwa haya si ya kutumia dawa kwani si magonjwa ya kuogopwa.
Haya ni magonjwa yanayotoka katika mfumo wa upumuaji ili
- kutoa taka sumu kwa njia ya upumuaji
- Kubadilika kwa hali ya hewa kama vile joto, baridi, vumbi, upepo n.k
Masikio, pua na koo zinawasha pamoja hivyo zinashirikiana na Antibodies (Kinga ya mwili) kutoa kemikali sumu taka.
Mtu anapomeza Antibiotics ili atibu hayo magonjwa atakuwa ameuwa Kinga ya mwili (Antibodies)
Hivyo kutokana na kuangamizwa kwa kinga ya mwili, mwili utakuwa unashindwa kupambana na magonjwa.
2. Sleeping pills (Dawa za usingizi)
Kulala kwa asili huleta afya nzuri, lakini ukilala kwa kutumia dawa za usingizi utakuwa umelala kwa lazima.
Mtu anaweza kumeza vidonge vya usingizi kwa malengo mbali mbali ikiwemo ni pamoja na;-
- Hupunguza maumivu
- Kuondoa mawazo
- Mwili kupumzika
Yafuatayo ni madhara ya kutumia dawa za usingizi
- Kupoteza hamu ya kula
- Kusahau
- Kuwa mtumwa wa dawa hizi
- Huleta msongo wa mawazo
- Kupoteza uwezo wa kufikiri
- Baadhi ya madawa ya usingizi yanaweza kumfanya mtumiaji kuwa na hasira, majonzi pia na woga kwa kuwa yana kiwango kikubwa cha hallucinogenic
3. Anti iflammatory (Dawa za kuchua)
Dawa hizi ni kwa ajili ya kutibu baridi yabisi, kuteguka, maumivu ya mgongo na viungo vingine.
Wengi hutumia dawa hizi kwa kujitibu baridi yabisi, maumivu ya mgongo na maumivu ya viungo hali ya kuwa magonjwa hayo hayatibiwi kwa dawa za kuchua.
Ukitaka kutibu magonjwa haya kwanza ni kujua sababu za magonjwa.
4.
Watu wengi hutumia dawa hizi kwa ajili ya kupunguza maumivu, lakini dawa hizi zina mchanganyiko ambao hutawala kafein (Caffein)
Baadhi ya madhara yatokanayo ya kutumia dawa hizi ni pamoja na;
- Kuzidi kwa maumivu baada ya dawa kuisha
- Maumivu ya kichwa (Hasa kutokana na Kafein)
- Kutopata usingizi
- Matatizo katika Ini
5. Steroids (Dawa ya pumu)
Dawa hii hutumiwa na wagonjwa wengi wa pumu ili waweze kupumua vizuri.
Hutumia dawa hii kwa njia ya sindano kupitia katika mishipa ya damu na wakati mwingine hutumia kwa kunywa.
Dawa hii ni hatari na ina maelekezo ya kutosha ila watu wengi hawayafuati.
Kwani;-
- Dawa hii inatumika kwa muda mfupi na ni kwa ajili ya kuleta pumzi kwa mgonjwa na sio tiba ya muda mrefu
- Mtu yeyote anayetumia dawa hii akipewa dawa nyingine hawezi kupona.
Haya ni baadhi ya madhara yake;-
i. Kuumwa sana kwikwi
ii. Kuwa na mafuta mengi mwilini
iii. Kukosa amani na kuwa na huzuni
iv. Kukosa usingizi
Thank u but ushauri Ni upi kwa wagonjwa wanaotumia antibiotics je waamie kwa tiba asili
ReplyDeleteWatumie KWA kiasi. Lakini pia ni vema kuzingatia kanuni bora za ulaji wa vyakula, matunda na kunywa maji mengi ili kupunguza sumu mwililini🙏🙏🙏
Delete