Kumbe hunitaki binti, yanini ulinichuna?
Ukadinya zangu senti, Kumbe upendo hakuna
Sasa I don't want, Kusikia lako jina
Kumbe si type yako, kwanini ulinichuna?
Najuta kukufahamu, Nimeshajiona boya
Japo dhambi kuhukumu, Ila wewe ni mala,,,,,,,
Nimeambukia sumu, nitaandika riwaya
Kumbe si type yako, kwanini ulinichuna?
Uliniona mshamba, jinga lilo mahututi
Kijana kodi ya nyumba, nikakulipia ETI
Kumbe huko unatamba, umenipata roboti
Kumbe si type yako, kwanini ulinichuna?
Ukanifanya kuruta, kuwa kwako cheo sina
Ukawa wanikokota, na vimaneno mwanana
Nilidhani nimepata, kumbe nimepatikana
Kumbe si type yako, kwanini ulinichuna?
Bila haya wala soni, Ukaanza nichubua
Mara pesa gulioni, zote mimi ninatoa
Nikikuomba vya ndani, mengi wajisingizia
Kumbe si type yako, kwanini ulinichuna?
Japo hali ime taiti, lakini nilijikaza
Nikakupeleka saiti, mali zangu kukujuza
Kwajili yako na fight, lengo wewe kukutunza
Kumbe si type yako, kwanini ulinichuna?
Ukiwa nami u mwema, unajifanya mpole
Ukitoka wanisema, kuninyoshea vidole
Kumbe lengo kunichuma, umepata MSUKULE
Kumbe si type yako, kwanini ulinichuna?
Umeshanichuna ngozi, sasa nimebaki kucha
Nazinduka usingizi, tayari kumeshakucha
Kuwa nawewe siwezi, kwa ulivo nipukucha
Kumbe si type yako, kwanini ulinichuna?
Nitampata mwenzangu, tutae endana kasi
Leo kwako neno langu, ni "MIMI NA WEWE BASI"
Japo nalia kizungu, bila kufuta kamasi
Nitampata mwenzangu, atakaye niridhia
Hii ni yako talaka, nimekwacha uelewe
Tabiazo nimechoka, nipe na maji ninawe
Mjinga akishituka, juwa mjinga ni wewe
Nitampata mwenzangu, atakaye niridhia

umetisha
ReplyDeletetunajaribu kiongozi wangu
Delete