Tunahimizana katika kuwahi kuamka na kwenda katika majukumu yetu ya kila siku.
Kijogoo kimewika, fumbueni macho yenu
Inapasa kuamka, Kunjeni na shuka zenu
Muda wa kuwajibika, humo makazini mwenu
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Mzungu na mwafrika, twendeni kibaruani
Muda wa kuchakarika, tajiri na masikini
Sisi njaa inanuka, hakuna kitu tumboni
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Mwalimu fanya haraka, uwahi kwenda shuleni
Fundisha kwa uhakika, wategemewa nchini
Japo una lalamika, mshahara wako duni
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Na mkulima zinduka, katie jembe mpini
Haraka shambani shuka, kuchimbua aridhini
Kwa weledi shughulika, usichoke asilani
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Boda boda WESE weka, na yule wa daladala
Kijiani tiririka, watoto wapate kula
Ajali zembe epuka, family haitokula
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Mama ntilie pika, tule tupate na nguvu
Matumbo yanachemka, Twahitaji utulivu
Usafi wahitajika, kaza utakula mbivu
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Ndugu zangu wa kandanda, kajiepushe na rafu
Mpira chako kiwanda, kanyaga tunakusifu
Afande zivae gwanda, husika na wahalifu
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Machinga chunga mipaka, fujo si pake mahali
Weka panapo husika, iheshimu serikali
Jiepushe na vibaka, watakufilisi mali
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Viti vya kuzunguuka, ndugu zangu vibosile
Punguzeni kubweteka, hizi sio enzi zile
Kijipu kitatumbuka, kaza buti songa mbele
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Najua sina lahaja, si mtunzi mashuhuri
Ipo siku nitakuja, kukupa tamu shairi
Hata na niso wataja, tushikamane ngangari
Kumekucha amkeni, mkatafute chochote
Inapasa kuamka, Kunjeni na shuka zenu
Muda wa kuwajibika, humo makazini mwenu
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Mzungu na mwafrika, twendeni kibaruani
Muda wa kuchakarika, tajiri na masikini
Sisi njaa inanuka, hakuna kitu tumboni
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Mwalimu fanya haraka, uwahi kwenda shuleni
Fundisha kwa uhakika, wategemewa nchini
Japo una lalamika, mshahara wako duni
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Na mkulima zinduka, katie jembe mpini
Haraka shambani shuka, kuchimbua aridhini
Kwa weledi shughulika, usichoke asilani
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Boda boda WESE weka, na yule wa daladala
Kijiani tiririka, watoto wapate kula
Ajali zembe epuka, family haitokula
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Mama ntilie pika, tule tupate na nguvu
Matumbo yanachemka, Twahitaji utulivu
Usafi wahitajika, kaza utakula mbivu
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Ndugu zangu wa kandanda, kajiepushe na rafu
Mpira chako kiwanda, kanyaga tunakusifu
Afande zivae gwanda, husika na wahalifu
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Machinga chunga mipaka, fujo si pake mahali
Weka panapo husika, iheshimu serikali
Jiepushe na vibaka, watakufilisi mali
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Viti vya kuzunguuka, ndugu zangu vibosile
Punguzeni kubweteka, hizi sio enzi zile
Kijipu kitatumbuka, kaza buti songa mbele
Amkeni kumekucha, siku mpya imeanza
Najua sina lahaja, si mtunzi mashuhuri
Ipo siku nitakuja, kukupa tamu shairi
Hata na niso wataja, tushikamane ngangari
Kumekucha amkeni, mkatafute chochote
COMMENTS