Unaweza kuondokewa na mtu muhimu na mambo yako kuyumba ukatamani bora arudi. Mtunzi anamlilia mmoja katika watu wake muhimu
Nimesema visikike, angalau kwa umbaliKwa
wanaume na wake, ali ala kulli haliTangu
baba uondoke, sinae wa kujadiliBaba rudi univike, medondosha sarawili
Umekwenda
wapi baba? Mbona hujaniarifuMwana
usawa wakaba, nalala kwenye sakafuNani
atakae ziba, pengo lako takatifuBaba rudi univike, medondosha sarawili
Tulipanga
mengi hasa, tutekeleze mi naweSi
maswala ya siasa, ni mambo yetu mi naweLeo
nimeshakukosa, uliko unieleweBaba rudi univike, medondosha sarawili
Umekwenda
wapi faza, miji yote sikuoniSi
Dodoma wala mwanza, kote haupatikaniMwanao
ninakuwaza, nijekutia machoniBaba rudi univike, medondosha sarawili.
Fikira
zinapishana, IBUN ni kwa babaeMebaki
moyo wanena, sina wakusema naeMajanga
yamepandana, sasa nani nimwambie?Rudi lau mara moja, nikunong’oneze
kitu.
Ulimwengu
ni mzito, bora mlima sayuniUlimwengu
ni wamoto, bora maji ya kunguniUlimwengu
ni mkato, wera wembe wa dukaniRudi lau mara moja, nikunong’oneze
kitu.
Yapo
mengi majaribu, yalonizidi umuriKila
siku naharibu, sijafanyha jambo zuriasa
naona aibu, kama lopata sifuriRudi lau mara moja, nikunong’oneze
kitu.
Baba
wapi umekwenda? Nikupe namba za simuUnitafute
huenda, nipunguze yangu hamuKama
upo GENDA GENDA, nimuagize ADAMURudi lau mara moja, nikunong’oneze
kitu.
Nalia
bila machozi, ni siri ya moyo wanguNaficha
hisia hizi, wasijue walimwenguHata
kwenye usingizi, nakuota ndugu yanguRudi tupange mipango, tuendeshe jambo
letu.
(tar 17.04.2017 – jumatatu saa 9:20
usiku wa manane)
NA; SAIDI BUNDUKI
COMMENTS