Huyu ni Mwanamke ambaye amechoshwa na tabia MBAYA za mumewe na anataka kurudi nyumbani kwao
1. Hu mume hu mtalaka, bwana ngoja nikuseme
Nasema nawe mkaka, ujionaye Gudume
Nadhani umenichoka, na imevunjika ngome
Ni kheri nirudi kwetu, hujanitoa mtini
2.Mwanzoni hukuwa hivi,umekuwaje mwenzangu
Umezidisha ugavi, najisikia uchungu
Imi siwezi ugomvi, Naomba twalaka yangu
Ni kheri nirudi kwetu, hujanitoa mtini
3. Hukuwa hivi awali, myaka sita ilopita
Pindi niko mwanamwali, Mzima ulinikuta
Kweli leo baba ALI, unanipeleka puta?
Ni kheri nirudi kwetu, hujanitoa mtini
4. Huyu salome ninani? Asifuye kazi yako
Hakuwachi asilani, Tena anaishi Keko
Nimepata walakini, Nimeumia mwenzako
Ni kheri nirudi kwetu, hujanitoa mtini
5. Zile Honey beby beby, zimepotelea wapi?
Mgongoni hunibebi, mashamsham hunipi
Nifanye nini ya Rabi, Nimeshakuwa makapi
Ni kheri nirudi kwetu, hujanitoa mtini
6. Kucha bize mitandao, ukiguswa u Mkali
Wakuhitaji wanao, unakua nao mbali
Na hata mimi mkeo, nahamu na wako mwili
Ni kheri nirudi kwetu, hujanitoa mtini
7. Twitter youtube na Tango, facebook waabudu
Namimi huna mpango, Ukilala ni kibudu
Naufunga huu mlango, ndoa ninaihusudu
Ni kheri nirudi kwetu, hujanitoa mtini
8. Mwaka sasa umekata, Sijui kipya kitenge
Wenzangu wana takata, wa buza kwa mpalange
Naona aibu hata, kwenye ya watu magenge
Ni kheri nirudi kwetu, hujanitoa mtini
9. Sio mume si wazimu, nimeshakuchoka zigo
Kama ndimu iwe ndimu, Kama zogo liwe zogo
Najua huna nidhamu,natarajia kipigo
Ni kheri nirudi kwetu, hujanitoa mtini
10. Namchukua mwanangu, narudi naye makwetu
Baki na hao machangu, na kurudi sithubutu
Na akuongoze Mungu, Uache na utukutu

Shairi zuri sana
ReplyDeleteHongera
Asante saaaana
Delete