Katika makala hii tutakufahamisha dawa sahihi kwa mwenye vidonda vya tumbo. Lakini pia dawa hatari zaidi

Nini vidonda vya tumbo, na zipi aina zake
Vidonda vya tumbo kitaalamu hufahamika kama ulcers, ni vidonda vinavyotokea kwenye tumbo. Vidonda hivi vimepewa majina mbalimbalu kulingana na aina zake. Vipo ambavyo huitwa gastric ulcers ambavyo ni vile avinavyotokea kwenye tumbo la chakula. Aina nyingine huitwa esophangeal ulcers hivi ni vile vinavyotokea kwenye sehemu inayojulikana kama esophagus, ni sehemu inayounganisha koo la chakula na tumbo la chakula. Na aina ya mwisho hujulikana kama duodenal ulcers hivi hutokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayofahamika kama duodenum.
Kwa siku za mwanzo ni ngumu kugundua kama una vidonda vya tumbo. Vipimo vinahitajika kugundua kama una vidonda vya tumbo. Kwa kuwa vidonda vya tumbo vina sababu nyingi na hutokea kidogo kidogo, basi hata matibabu yake yanaweza kuchelewa. Endelea na makala hii hadi mwisho, nitakujuza vipimo vipi hutumika kutibu vidonda vya tumbo na ni matibabu gani yanahitajika kulingana na aina ya vidonda na sababu za kutokea kwake.
Vipimo vya vidonda vya tumbo:
Vipimo vya vidonda vya tumbo vimegawanyika katika makundi mengi. Na hata gharama za vipimo vyake zinatofautiana kulingana na kipimo kilichotumika. Hivyo kaama una dalili za vidonda na umepima huna mbadala wa aina nyingine ya kipimo.
Aina hizo ni kama:-
(i) Aina ya kwanza ya kipimo ni ila ambayo lengo lake kubwa ni kuchunguza kama ndani ya tumbo kuna bakteria aina ya H.pylori. Hawa ndio bakteria ambao wanasababisha vidonda vya tumbo kwa kiasi kikubwa. Vipimo hivi mara nyingi ni kwa njia ya kinyesi. Hata hivyo vinaweza kufanyika kwa njia ya pumzi (hewa) ama damu lakini njia hizi sio sahihi kuliko kwa kutumia kinyesi
(ii) Kwa kutumia kifaa cha kuingiza tumboni kinachojulikana kama endoscope. Hiki hungizwa ndani ya tumbo kisha humulika kama katochi. Kwa msaada wa kifaa hiki vidonda vya tumbbo vinaweza kuonekana kwa macho
(iii) Kwa kutumia x-ray hii ni x-ray maalum kwa lengo la kuchunguza safu za juu za tumbo. Kipimo hiki pia hufahamika kwa jina la barium swallow.
Matibabu na dawa za vidonda vya tumbo:
Kama ulivyojifunza huko juu kuwa matibabu ya vidonda vya tumbo hutolewa kwa kulingana na aina ya vidonda na kulingana na sababu zake. Kama sababu ni bakteria mgonjwa atapewa dawa za kuuwa bakteria. Kama sababu ni ongezeko la tindikali tumboni mgonjwa atapewa dawa ya kupunguza uzalishaji wa tindikali tumboni.
Dawa za vidonda vya tumbo ni kama:-
(a) Dawa za kuuwa bakteria wanaosababisha vidonda vya tumbo. Dawa hizo ni kama
Amoxicillin (amoxil)
Cacithromycin (Biaxin)
Metronidazole (flagyl)
Tinidazole (tindamax)
Tetracycline (tetracycline HCL
Levofloxacin (levaquin)
(b) Dawa za kuzuia uzalishwaji wa tindikali za tumboni. Dawa hizo ni kama:-
Omeprazole,
lansoprazole,
Rabeprazole
Esomeprazole
Pantoprazole
(c) Dawa za kupunguza uzalishwaji wa tindikali tumboni. Hiki ni kama
Ranitidine
Famotidine
Cimetidine
Nizatidine
(c) Dawa za kulinda ukuta laini wa tumbo hizi hujulikana kama cytoprotective agent. Dawa hizi ni kama sucralfate na misoprostol
Dawa mbadala za vidonda vya tumbo.
Tofauti na dawa hizo lakini pia vidonda vya tumbo vinaweza kutibiwa na tiba mbadala. Kuwa makini sana na tiba hizi kwa sababu hazina vipimo maalumu. Tiba hizi mara nyingi hufanya kazi vyema kama sababu ya vidonda ni bakteria. Lakini kama sababu ni nyingine tiba hizi sio sahihi sana.
Tiba hizi hujumuisha
Karoti, kabichi na bamia (hizi unaweza kutengeneza juisi yake).
Asali
Kitunguu thaumu
Shubiri
Athari za kutotibu vidonda vya tumbo:
Ugonjwa wowote unaweza kuwa na madhara zaidi endapo utachelewa kutibiwa. Hali hii pia ni kwa vidonda vya tumbo. Endapo havitatibiwa hadi athari mbaya zaidi inaweza kutokea. Ni kawaida kwa vidonda vya tumbo kusababisha kifo ila kama havitatibiwa mwisho wake unawez ukawa kifo.
Hebu tuone athari za kutotibu vidonda vya tumbo:-
* Kuvuja kwa damu ndani ya tumbo.
Damu hii unaweza kuiona kwenye kinyesi ama kinyesi kuwa cheusi sana ama kuwa na damu. Hali kama hii inaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini.
Chakula kinaweza kupita bila ya kumeng’enywa. Kutokana na kuwepo vidonda kwenye utumbo mdogo, chakula kinaweza kupita hata bila ya kumeng;enywa na kuingia kwenye damu kwa ajili ya kutumika mwilini. Endapo hali kama hii itatokea mtu anaweza kushiba kwa haraka sana na anaweza kupoteza uzito kutokana na kukosa virutubisho.
Pia vidonda vya tumbo visipotibiwa vinaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa mengine tumboni.
Vinaweza kupelekea utumbo kukatwa. Yes endapo eneo la jeraha limekuwa kubwa na gumu kutibika tiba mbadala ni kuondoa kipande cha utumbo kilichoharibika.
Mambo hatari kwa mwenye vidonda vya tumbo:
Kunywa pombe
Kuvuta sigara
Kula vyakula vyenye uchachu sana
Kuwa na misongo ya mawazo
Kukaa na njaa kwa muda mrefu
Kula vyakula vyenye pilipili kwa wingi
Kula vyakula vyenye chumvi sansa
Tukutane makala ijayo tuakapoangalia kuhusu dalili za minyoo na sababu zake.
COMMENTS