Je ni vipi na wapi naweza kupata minyoo? Na je Minyoo inatibika?? - SOMA MAKALA HII MPAKA MWISHO

Minyoo ni katika viume wanyonyaji, wanaoishi katika miili ya viumbe hai na kujipatia chakula humo. Minyoo wanaweza kuishi kwenye maeneo yenye majimaji kama kwenye maji, ndani ya viumbe hai kama mtu, ngombe, ngurue na paka. Minyoo pia wanaweza kuishi kwenye udongo.
Minyoo wanaweza kusababisha maradhi ndani ya mwili wa kiumbe hai. Minyoo isipotibiwa inaweza kusababisha athari zaidi kwenye afya ya mtu.
Makala hii inakwenda kukuletea dalili za minyoo.
Aina za minyoo:
Kuna aina za minyoo zipatazo 300,000 na kati ya hizo 300 tu ndio ambazo husababisha maradhi kwa binadamu. Minyoo imegawanyika katika aina kadhaa kulingana na tabia zao, jinsi wanavyozaliana na maeneo wanayoishi, pia na maumbile yako.
Aina hizo za minyoo ni kama:-
Trichinosis
Hawa tunaweza kuwapata kutoka kwa wanyama
Pinworm (thread worm)
Hawa ni wadogo sana na unaweza kuwapata kwa kuyala mayai yao kutoka pale yalipo. Kama utakuwa unanawa mikono mara kwa mara, kabla ya kula na huna tabia ya kula vidole ni ngumu kuwapata hawa minyoo.
Hookworm (roundworm) minyoo hawa husambazwa kupitia udongo na kinyesi.
Fluke; (flatworm) hawa wanaishi kwenye utumbo mdogo na meneo mengine. Tunaweza kuwapata kwenye vyakula na mboga zisizooshwa vyema.
Tapeworm (flatworm) unaweza kuwapata hawa kwenye maji machafu na kwenye vyakula.

Je ni wapi naweza kupata minyoo?
Minyoo tunaweza kuipata maeneo mengi. Na katika miili yetu pia inaweza kuingia kupitia njia nyingi. Njia kuu ni kwa kupitia mdomoni kwa njia ya chakula, ama kinywaji. Lakini pia inaweza kupitia kwenye ngozi. Hebu tuyaone maeneo ambayo monyoo ipo sana.
- Kwenye majimaji
- Ndani ya maji
- Kwenye udongo
- Kwenye nyama
- Kwenye chakula kisichopikwa kama matunda
- Kwenye mbog za majani
Ni kivipi naweza pata minyoo?
kwa kugusa kitu chenye mayai ya minyoo, kisha ukapeleka mkono mdomoni bila ya kuosha
Kunywa maji yenye mayai ya minyoo
Kula chakula chenye mayai ya minyoo
Kula udongo wenye mayai ya minyoo
Unapotembea bila ya viatu maeneo machafu
Unapokula vyakula visivyopikwa ama vilivyopikwa kwa uchache kama nyama ya ngurue.
Ni ziipi dalili za minyoo?
Maumivu ya tumbo
Kuharisha, kutapika na kupata kichefuchefu
Tumbo kujaa gesi ama kuunguruma
Uchofu wa mara kwa mara
Kupunguwa uzito bila ya sababu maalimu
Tumbo kujaa na kuwa gumu
Ni vipi naweza kuepuka kupata minyoo?
Osha mikono kabla ya kula ama kuingiza mdomoni
Kula chakula kilichopikwa vyema
Usile matunda bila ya kuosha
Unapotembea kwenye ardhi chafu usitembee bila ya viatu
Kama unaishi na paka ama mbwa hakikisha yupo salama
Vinyesi vya wanyama kama paka, mbwa, na wanyama wafugwo wa nyama vihifadhiwe vyema.
Kuwa makini na nyama ya nguruwe.
JE minyoo inatibika?
Ndio mimnyoo inatibika tena kwa muda mchache tu. Kama unasumbuliwa fika kituo cha afya kwa vipimo zaidi. Makala inayofata tutazungumzia kuhusu matibabu ya minyoo.
COMMENTS