Pa pa pa, ndani ya sekunde 30 - dakika 1 mzee ushamaliza. Unaiona dunia yote imekuelemea na hujui cha kufanya. MAKALA HII NI MSAADA KWAKO
Kuwahi kufila kileleni ni kupi?
Nimeamua kukupa njia na tiba ya kumaliza tatizo hili la fedheha hasa kwa kijana. Lakini kabla ya kuangalia njia za matibabu na suluhisho tuangalie kwanza vyanzo vya tatizo.
‘Kama unapenda kujifunza kuhusu
utalii wa ndani basi nikukaribishe kuitembelea channel yetu ya BUNDUKI TV
ambayo ni sehemu pekee itakayokujuza mengi na kukata kiu yako. BOFYAHAPA’
Sababu za kuwahi kufika kileleni (mwanaume)
Ziko sababu za kibaiolojia na za kisaikolojia. Ila nitakuambia zote kwa pamoja.
Sababu za asili / kurithi
Hizi ni sababu za kuzaliwa, ni aina ya watu ambaye amezaliwa na tatizo hili au amerithi kutoka kwa wazazi wake. Kwa tatizo hili ni vema kumuona daktari wa masuala ya afya ya uzazi kwa maelekezo zaidi.
Kutarajia kufeli
Wengine hutawaliwa na hofu kabla ya tendo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo huenda alishawahi kufeli siku za nyuma kabla.
Ugeni kwa mwanamke husika na mazingiza vinaweza kuchangia kuongeza hofu.
Kujichua (Punyeto)
Tulishaelezea kwa kina kuhusiana na madhara ya kupiga punyeto. Na hii ni miongoni mwa madhara yake makubwa, unajua ni kwanini?
Kwa sababu kujichua mtu huwa anajikadiria mwenyewe na pia mkono hauna joto kama ilivyo kwa mwanadamu. Hivyo anapokuwa na mpenzi ni ngumu kuweza kujizuia kufika kileleni kwa haraka kutokana na kuzoea mkono wake.
Papara uwanjani
Mwanamke umemfukuzia kwa muda mrefu bila mafanikio, siku unampata unakuwa unawaza moja kwa moja penzi lake na hatimaye ndani ya dakika moja unakuwa umeshamaliza au hata kabla ya kuanza (kwa baadhi yao).
Kukaa muda mrefu bila kufanya mapenzi
Hii
inatokana na kujaa kwa kibubu cha manii (shahawa). Siku ukikutana na mwanamke
inakuwa sio rahisi kutumia hata dakika 3. Inamaana chini ya dakika mbili
unakuwa umeshajimaliza.
Hili linakuwa sio tatizo sana kama utaweza kuendelea na kudumu na tendo.
Staili ya mapenzi
Kuna
baadhi ya staili ambazo humchochea sana mwanaume kuwahi kumaliza kutokana na
staili hizo kuwa na msisimko wa hali ya juu. Ziepuke katika raundi ya kwanza.
Sina haja ya kuzitaja hapa.
Msongo wa mawazo
Maisha yanatuadhibu katika njia mbali mbali. Kiasi ambacho hupelekea kuathiri hata mahusiano yetu na wenzetu.
Epuka sana kukaribisha mawazo potofu wakati wa tendo, mwisho wa siku unaweza ukawa kama sanamu lakini akili haipo mahala hapo na kujikuta unamaliza bila hata kujielewa na kutomtendea haki mwenzi wako.
Kuangalia picha za ngono (porn)
Kuna wanandoa huwa na utaratibu wa kuangalia picha za ngono aidha wakiwa pamoja au mtu akiwa peke yake.
Hii
hatari yake ni kwamba unaweza kumuwaza mtu uliyemuona katika picha na
akakuvutia kuliko mwenzi wako. Hatimaye wakati wa kufanya mapenzi ukajikuta
unawaza maumbile na utundu uliouona kwenye video ya ngono na hatimaye unamaliza
kabla ya muda wa mweza kuridhika.
SULUHISHO
- Fanya mazoezi
- Muandae mwanamke kabla ya kumuingilia
- Usiwaze sana tendo wakati unafanya
- Jifunze kurudisha mkojo
Fanya
mazoezi ya kubana mkojo wakati unakwenda kukojoa mkojo wa kawaida. Ubane kwa
sekunde kadhaa kisha uachie. Fanya hivyo kila unapokwenda haja ndogo. Utazoea
na utaweza kubana manii wakati wa kungonoka.
- Wacha punyeto
- Punguza kula vyakula vinavyoongeza hisia
- Kama umeoa usikae muda mrefu bila kufanya
- Epuka / Acha kuangalia ngono
- Kula chakula bora na matunda
- Zungumza na mwenzako
- Usianze na staili tata kwako
- Fika hospitali / waone wataalamu wa afya ya uzazi.
Madhara ya mwanaume kuwahi kufika kileleni
Kudharaulika
Jamani dharau ni mbaya asikwambie mtu. Hasa kudharauliwa na mtoto wa kike kwa sababu umeshindwa kumridhisha.. Daaah acha tu. Na hiyo inapelekea sababu namba mbili hapa chini.
Mwanamke kuchepuka
Kama unadumu kwa muda mrefu na mwanamke bila kumridhisha unatarajia nini kitatokea? Ukizingatia wanawake wenyewe wameshapita sehemu mbali mbali kwahiyo wanajua mwanaume kamili anakuwaje na mwanaume mgonjwa nakuwaje. Hapo tarajia kukimbiwa ndugu yangu.
Kibaya zaidi ni kupelekea sababu namba tatu hapo chini hutokea.
Stress
Mbali na stress zako za kukosa pesa, hatimaye unaongezewa stress za mapenzi kwa kuona mwanamke wako ana mwanaume mwengine kama sio kukukimbia kabisa au kukuibia haki yako.

Unadhani ninikitatokea baada ya hapo? Ni sababu namba nne hapo chini.
Kuvunjika kwa ndoa / mahusiano
Hakuna mwanamke anaweza kuvumilia kukaa na mwanaume ambaye hamridhishi. Atavumilia lakini mwisho atachoka. Asipovunja mahusiano yenu basi atakufanya wewe uvunje mahusiano au ndoa hiyo.
Mbali na hayo, madhara mengine ni pamoja na;-
- Hasira za mara kwa mara kwa mwanamke
- Kusababisha ugonjwa wa moyo kwa mwanamke kwa kutofikishwa kileleni
- Mwanamke kubaki na maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Mwanamke kuchukia tendo la ndoa
- Kukosa usingizi
Hitimisho
Ingawa hatufanani lakini jitahidi kadiri ya uwezo wako kuhakikisha unakamilisha vema na mwenzi wako tendo hili la asili na la uumbaji wa Mwenyezimungu. Ukimbiwe kwa sababu nyingine lakini sio kwa shoo mbovu.
Uwe na siku njema ndugu msomaji
TUNAKUPENDA
COMMENTS