Tangawizi ni mmea ambao ni jamii ya maua. Mizizi ndiyo hasa hutumika kama viungo katika vyakula lakini pia hutumika kama tiba asili. Tangawizi ni mmea ambao hustawi sehemu mbali mbali duniani
Hapa chini nimekuwekea mmea wake ili uweze kuufahamu.
Mmea wa tangawizi |
Mbali na kuwa ni chakula kitamu, hasa ikiwekwa katikamchanganyiko wa chai, lakini hapa tutazungumzia matumizi yake kama tiba.
- KUONDOSHA MAUMIVU
Utomvu wa tangawizi umeonekana kusaidia sana katika kuondosha maumivu katika sehemu mbali mbali za viungo vya mwili.
Chua kwa kutumia utomvu huu mara mbili kwa siku katika sehemu ambayo inauma (maumivu ya misuli) kama vile magoti, maumivu ya kichwa na kadhalika.
- KOO KUKEREKETA
Kuwashwa kwa koo, kitaalamu huitwa (sore throat) na pia hutibu ugonjwa wa mafua. Unaweza kutafuna kipande kidogo cha tangawizi.
- HUZUIA KUTAPIA NA KIZUNGUZUNGU
Tafiti zimeonyesha kuwa tangawizi ina uwezo mkubwa katika kuondosha homa za kutapika na kizunguzungu (motion fever) kwa wasafiri wa vyombo vya majini, nchi kavu na hata angani
- Tafiti mbalimbali ulimwenguni zimethibitisha tangawizi kuwa na uwezo mkubwa katika kuondosha homa za kutapika na kizunguzungu (motion fever) kwa wasafiri wa vyombo mbalimbali baharini na nchi kavu.
- Pia huondosha kichefuchefu na kutapika kwa akinamama wajawazito na hata kwa wagonjwa wanaofanyiwa operesheni. Inasadikika kijiko 1 cha tangawizi iliyosagwa kinatosha kumuondolea kichefuchefu na kutapika mgonjwa baada ya kufanyika operesheni.
- Tangawizi pia imegundulika kupunguza kwa kiasi kikubwa lehemu katika mishipa ya damu na kuzuia damu kuganda katika mishipa hiyo, hivyo kuzuia kutokea madhara ya kuziba kwa mishipa ya damu jambo ambalo linazaweza kusababisha maradhi ya moyo na kupooza kwa viungo vya mwili.
- Tangawizi pia imegundulika kuwa dawa muhimu kupunguza au kuondosha kabisa maumivu wanawapata kinamama wengi wakati wa hedhi.
- Vilevile tangawizi imedhihirisha kuwa na uwezo mkubwa kuponya haraka maumivu makali ya tumbo yanayowapata mara kwa mara watoto wadogo.
- Katika baadhi ya nchi tangawizi inatumika katika kuhifadhi chakula kwa muda mrefu, hii inatokana na ukweli kwamba ina uwezo mkubwa wa kuua aina nyingi za bakteria kama vile E.coli, Salmonella na wengine wengi ambao huharibu vyakula vyetu.
- Tangawizi hukiamasisha kimengenyo mwilini kilichopo mwetu kiitwacho Gastric juice kufanya kazi ipasavyo na hivyo husaidia kuzalisha joto la mwili ambalo huwapa nafuu wagonjwa wengi wa mafua na maumivu ya tumbo.
- Watu wengi ulimwenguni hutumia mmea huu kama dawa ya kuondoa harufu mbaya kinywani.
- Hutumika katika utengenezaji wa siki (vinegar) ambayo huamasisha hamu ya kula.
- Pia husaidia kushusha presha ya damu mwilini (hypertension) kwa watu wanaosumbuliwa na presha ya kupanda.
- Tangawizi pia hutumika kupunguza maumivu yanayosababishwa na matatizo ya mawe kwenye figo, vilevile hupunguza maumivu ya kibofu cha mkojo iwapo itatumika kuchuliwa kwa nje sehemu za mwili zilizo karibu na kiungo hiki.
- Virutubisho vilivyomo kwenye zao hili pia huhamasisha utendaji mzima wa vimengenyo mbalimbali katika usagaji wa chakula mwilini
Lakini itabidi izingatiwe kwamba isitumiwe kwa watoto chini ya miaka 2, itumiwe kwa watoto zaidi ya umri huo kuwaondolea adha kama vile za kuumwa vichwa, kichefuchefu na kuumwa matumbo.
Dozi ya tangawizi itolewe kulingana na uzito wa mtoto husika. Dozi nyingi za dawa za mitishamba hutolewa kwa kulinganishwa na dozi ya mtu mzima wa kilo 70, hivyo mtoto wa kilo 20 hadi 25 hupatiwa 1/3 ya dozi ya mtu mzima. Kwa ujumla kwa dozi ya mtu mzima huwa isizidi gramu 4 kila siku.
HITIMISHO:
Ni vyema tukajenga mazoea ya kutumia dawa zitokanazo na mimea kama tangawizi kwa ajili ya kinga na tiba mbalimbali za miili yetu kwa sababu licha ya kuwa zinapatikana kirahisi pia si ghali na hazina madhara yeyote kwa afya zetu kama zilivyo dawa nyingi za viwandani.
Mimi natafuna tangawizi kila siku, naona imesaidia kulainisha choo na kupumua
ReplyDeleteAsante sana kwa kuwa nasi
DeleteAta mm natafuta tu inansaidia sana
ReplyDelete