Jitibu nyumbani kwako matatizo ya mba kwa kutumia mmea huu maarufu
_________________
Leo nakupa njia nyepesi na rahisi ya kujitibu m ba hapo hapo ulipo.
Bila shaka unaufahamu mmea maarufu wa shubiri (aloe vera). 'Naam' basi mmea huu ni tiba kwa magonjwa mengi ikiwemo tatizo hili la mba.
JINSI YA KUFANYA
Chukua majani ya aloe vera kisha limenye vizuri na ulikate kate vipande vidogo vidogo halafu lisage kwa kutumia brenda au liponde kwenye kinu hadi upate uji uji.

Chuja vizuri uji huo kutoa makapi kama picha inavyoonekana hapo juu. Kisha chukua mafuta yoyote ya kupaka na uchanganye na uji uji wa ile shubiri yako.
Hakikisha mchanganyiko ule unakuwa sawa sawa, mafuta yasizidi sana wala shubiri isizidi sana.
Hakikisha nafuta unayotumia hayana kemikali kali sana kama losheni wanazotumia baadhi ya wanawake kujichubua. Ni vema uukitumia mafuta ya nazi.
DOZI
Tumia mchanganyiko huo kujipaka sehemu iliyoathirika au kama ni mwili mzima jipake mwili wote. Tumia dozi hiyo kwa siku mara mbili asubuhi na muda wa kulala.
Tumia dozi hiyo kwa muda wa siku saba mpaka siku 14 kulingana na ukubwa wa tatizo.
Kabla ya kupaka sehemu iliyoathirika hakikisha kuwa unaisafisha vizuri kwa maji na sabuni.
Asante kwa kusoma makala zetu. Tutakutana wakati mwingine kwenye makala nyingine.
Soma pia
Mabadiliko ya rangi za Mkojo na maana zake
Vyakula hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo
******************
COMMENTS