Wasiliana na Mwandishi wa Makala hii kwa namba - 0625 71 80 40

1. (NEWS) HABARI
2. TOURS (SAFARI)
3. AFYA
4. TEKNOLOJIA
Katika upande wa teknolojia unaweza kuzungumzia kuhusu masuala mbali mbali ikiwemo habari mpya zinazohusiana na simu, kompyuta na kadhalika.
Watu wanapenda kujua undani wa vitu vinavohusiana na teknolojia, watu wanataka kujua kuhusu kuzuia virusi katika simu zao, program mpya na mambo mengine mengi kwani segment hii ni pana mno.
Tazama
Ujio wa simu mpya ya infinix NOTE 9
5. MAPISHI
Unaweza kupika?
Basi watu wengi wanapenda kula vizuri na kupika vyakula vipya kila siku. Kama una utaalamu juu ya mapishi anza sasa kuwafundisha watu.
Wanawake wengi wanapenda kupika lakini hawana walimu wa kuwafundisha ama kuona aibu kwenda kwa wataalamu. Hivyo atakapoingia katika channel yako atakuwa anajifunza mwenyewe kadiri ya uwezo wake.
6. VICHEKESHO
Kuna muda tunapenda kufurahi na kucheka ili kusahau shida zetu.
Je wewe una kipaji cha kuchekesha? Basi unaweza kukitumia kwa kurekodi clip zako na kuziweka youtube kisha tukazifurahia.
7. MAPENZI NA MAHUSIANO
Watu kila siku wanakuwa na kuingia katika mahusiano.
Watu kila siku wanaachwa na kuumizwa. Lakini pia sambamba na hilo watu huhitaji kuingia katika mahusiano mapya na kuhitaji ushauri wa kumaliza mawazo yao yanayowaumiza.
Kama utakuwa na elimu juu ya mapenzi, ndoa, mahusiano ni wakati wako sasa kuleta darasa hilo katika ulimwengu wa mtandao kila siku.
8. UMBEA WA WATU MAARUFU
Kama ijulikanavyo kuwa watu maarufu kama vile wasanii, wanasiasa, wafanya biashara nk huwa na watu wengi nyuma yao ambao huwapenda na kuwasikiliza. Mashabiki wao hufuatilia sana maihsa ya mastaa wao.
Hivyo basi kila kukicha wanapenda kusikia mapya kuwahusu. Yawe mazuri, mabaya au katika mtiririko wa kazi na maisha yao ya kawaida.
Kama una uwezekano wakupata habari zao kila siku hii ni sehemu nzuri ya kujipakulia maujiko kutoka kwa watumiaji wa mtandao wa youtube.
9. MUSIC
Kama una kipaji cha kuimba unaweza kuutumia mtandao wa youtube kuwaburudisha watu. Fungua channel ya youtube na uweke kazi zako huko.
10. MUSIC UPDATES
Mbali na kuimba, pia unaweza kujihusisha na uchambuzi wa muziki mpya kutoka kwa wasanii mbali mbali. Unaweza kutoa ufafanuzi wa mziki kwa ujumla kama vile video, audio, washiriki, udhaifu ama ukubwa wake.
Hii inaweza kuambatana na kutoa kasoro ambazo zipo kwenye wimbo wa msanii sambamba na kuutangaza ukubwa wake aidha katika nchi husika ama dunia kwa ujumla.
11. MUSIC COVER
Hapa pia ni kwa mwenye kipaji cha kuimba. Lakini cover ni kitendo cha kuimba nyimbo ya mtu mwingine kwa mara nyingine.
Watu kadhaa wamefaulu katika hili baada ya kuonekana na watu maarufu wakiwa wanaimba cover za watu hao.
12. DANCING (KUCHEZA)
Inataka kufanana na music cover lakini hapa utakuwa unajihusisha na kucheza tu. Hizi ni miongoni mwa burudani ambazo watu hupenda sana hasa baada ya msanii mkubwa kutoa nyimbo.
Ukicheza vizuri una asilimia kubwa ya kuliteka soko la burudani hasa kwa wapenzi wa mziki mzuri.
12. INTERVIEWS
Hapa unaweza kujihusisha sana na interview za watu maarufu. Watu wanapenda kusikia mengi kutoka kwa watu wao.
Mfano wa watu ambao hufanya vizuri sana katika interview za watu maarufu ni pamoja na channel ya YAH STONE TOWN ya Salama Jabir na ZAMARADI TV na nyingine nyingi.
14. MIKASA YA MAISHA
Tunajua wazi kuwa maisha ni safari ndefu na watu wengi hupitia magumu. Yapo ya kujifunza, kustaajabisha na hata kuelimisha sambamba na kuburudisha.
Yapo ya kutisha ambayo watu hupitia kiasi kwamba huwezi kuamini mpaka utakapo mpata mhusika akakusimulia.
Visa na mikasa ni miongoni mwa vitu ambavyo watu wengi wanapenda kusikia. Unaweza kujikita katika tasnia hii na kuwatafuta watu wa aina hiyo.
Mfano wa channel zinazofanya vizuri katika upande huu ni pamoja na DAVISTA MATA MEDIA na BUNDUKI TV
15. UNBOXING
Unboxing ni kitendo cha kufungua bidhaa mpya.
Tunafahamu kuwa kila siku kunatoka bidhaa mbali mbali mpya. Unaweza kuiwahi fursa hii na kuzama sokoni kuangalia kuna kitu gani kipya na ukakifikisha kwa raia kabla hawajapata maamuzi ya kukinunua.
Inaweza kuwa ni simu, kompyuta, tv na vingine vingi. Hii itapendeza zaidi kama utakuwa unawaeleza watu uimara wake na udhaifu wake ili wafahamu vema kabla ya kufanya maamuzi.
Leo wacha tuishie hapa ili nikupe nafasi ya kusubiri sehemu ya pili ambayo tutamalizia niches 11 zilizobaki.
Una maoni yoyote, ushauri au maswali?
Shuka chini sehemu ya comment na utuandikie nasi tutayapitia.
Asanteni sana
ReplyDelete