Mara tu uonapo dalili hizi, fahamu kuwa una upungufu wa damu. Wahi kwa wataalam wa Afya

Hii ni kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali, ujauzito, hedhi nzito, magonjwa sugu na lishe duni yanye upungufu wa madini ya folic, madini ya chuma na vitamin B12
Dalili hizi zitakufanya utambue kama unakabiliwa na tatizo hili;-
1. Kuchoka sana
2. Maumivu makali ya kichwa
3. Kupungua kwa uwezo wa kufikiria
4. Sehemu nyeupe ya jicho kuwa bluu
5. Kushindwa kupumua vizuri
6. Vidonda kwenye ulimi
7. Miguu na mikono kuwa ya baridi sana
8. Kucha kuwa dhaifu
9. Ngozi kupauka na kuwa na rangi ya kijivu
10. Hasira kupita kiasi
Matibabu ya upungufu wa damu
Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamin C na vitamin B12 sambamba na madini ya chuma.
Pia wakati mwingine vidonge na sindano zenye lishe hizi huweza kutumia hospitali na matibabu ya tatizo hili.
Mgonjwa anapokuwa ameshaathirika kwa kiasi kikubwa huweza kuongezewa damu moja kwa moja.
Safi sana
ReplyDelete