BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM MWENYE KUSIKILIZA QUR'ANI Imepokelewa kutoka kwa Mohammad bin bashiir [1] kutoka kwa Ali bi...
BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
MWENYE KUSIKILIZA QUR'ANI
Sisemi kwa kila aya lakini kwa kila herufi sawa iwe baa au faa au mfano wa hizo, akasema: Na mwenye kusoma herufi moja hali ya kuwa amekaa kwenye sala, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi hiyo mema khamsini, na kumfutia makosa khamsini, na kumuinua daraja khamsini, na mwenye kusoma herufi moja hali ya kuwa amesimama kwenye sala yake, Mwenyezi Mungu humuandikia mema mia moja na kumfutia makosa mia moja na kumuinua daraja mia moja, na mwenye kuihitimisha, maombi yake ni yenye kukubaliwa, sawa yachelewe au yawahi akasema: Nikasema: Niwe fidia yako mwenye kuihitimisha yote? Akasema: Mwenye kuihitimisha yote.[2]
Na imepokelewa kutoka kwa Is'haq bin Ammar, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s) amesema: Mwenye kusoma aya mia moja akisali kwa kisomo hicho kwa usiku mmoja Mwenyezi Mungu humuandikia kwa aya hizo kunuti za usiku na mwenye kusoma aya mia mbili tofauti na kwenye sala ya usiku Mwenyezi Mungu humuandikia kwenye lauhul mahfuudh mema yaliyo sawa na mali nyingi (qintwaar ) na qintwar ni kinaya ya mali nyingi, aukia miamoja, na awqiyah ni kubwa zaidi ya mlima wa Uhudi.[3]
Na imepokelewa kutoka kwa Anas amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w): Mwenye kusoma aya mia moja, hataandikwa miongoni mwa wenye kughafilika, na mwenye kusoma aya mia mbili huandikwa miongoni mwa wenye kunyenyekea na watiifu, na mwenye kusoma aya mia tatu Qur'ani haitamtolea hoja, yaani mwenye kuhifadhi kiwango hicho cha aya za Qur'ani, husemwa: Hakika mtoto amesoma Qur'ani: Kwa maana amehifadhi.[4]
imenakiliwa na sayyidbunduki.blogspot.com
kutoka katika vyanzo vinavyoaminika
COMMENTS