Palo kunjufu nakunja, sikizeni kwa makini
Usionje na kuonja, kakataza Rahimani
Kileo chochote kile, amekataza Jalia
Usipapukie papu, ukipewa ikataa
Ile ya matapu tapu, boha pingu na chang’aa
Licha kunguza mapupu, unaweza jichafua
Ni katazo la Mwenyezi, pia dhara kwa jamii
Ni m baya uraibu, mengi umesha yaona
Kuna ile ya zabibu, japo ni tunda mwanana
Acha zile za warabu, wazungu pia wachina
Katazika mwanadamu, pombe inaangamiza
Majina hadi karaha, zidi ya kumi na saba
Kuna ino itwa boha, na sasa kuna viroba
Zote huvuruga siha, mwisho upelekwe soba
Wamezipamba majina, lakini zote haramu
Kuna ya enzi na enzi, harufu kama ya choo
Ile pombe ya mnazi, kwa jamii si kioo
Rafiki zake ni inzi, inalewesha mnoo
Epuka hata kuonja, laana yake ni kubwa
Wamezivika majina, hasa hizo pombe kali
Kuna hiyo SENTI ANNA, chupa moja tumbo chali
Sijui kuna Banana, na hiyo nayo ajali
Jamani tuzindukeni, pombe ni hatari sana
Usinywe pombe kijana, ni haramu haifai
Kama una kiu sana, kunywa soda, kunywa chai
Huo sio uvulana, kwa jamii ni adui
Usipo kunywa kilevi, utapasuka kibofu?
Natia nanga NGANGANGA, japo mbaya maudhui
Kama losema ujinga, kwako takuwa adui
Ila kuhusu kutunga, kwakweli bado sijui
Malenga munikosoe, pale penye hitilafu
Shairi mekosa jina, kwa uchache wa ilimu
Hivyo basi waungwana, naomba munikirimu
Pendekezeni majina, lipi litakuwa tamu?
Jina gani ngependeza, kuita shairi hili?

COMMENTS