Yowe langu
kigong’ondo, sikia pwani na bara
Wasikie wa
Kibondo, Lindi mpaka Mtwara
Wasikie
walo kando, dimbwini na bara bara
Usiombe
yakukute.
Kufumaniwa kwauma,
sikilia kwa wenzio
Unaweza ukazima,
kwa kupigwa na pumbao
Wengine hupigwa
chuma, kupoteza utu wao
Usiombe
yakukute.
Usiombe kuchawiwa,
kwa sababu ya mapenzi
Mijidawa kuwekewa,
unyunyu kwenye mchuzi
Wallahi utapagawa,
kupelekwa kama mbuzi
Usiombe yakukute.
Usiombe ukaachwa,
na yule unompenda
Hapo utaona
kichwa, chawasha kama kidonda
Kila jua
likikuchwa, wakichukia kitanda
Usiombe yakukute.
Kuoa uso
mtaka, mke wa kulazimishwa
Ile ndoa ya
mkeka, siku ulo furumushwa
Nafsi itakauka,
kama papa lo kaushwa
Usiombe yakukute.
Kuibiwa ni kubaya,
kile uno kithamini
Mda mrefu
wagwaya, kukipata cha moyoni
Leo BOYA
bila haya, kakitia mikononi
Usiomba yakukute.
Leo umetimamia,
viungo vyote mwilini
Kwa madaha
watembea, kujivuna majiani
Usiombe kuumia,
kupoteza vya mwilini
Usiombe yakukute.
Ulikuwa una hela, wala wavaa wadunda
Masikini kwako fala, chapa fimbo kama punda
Kuamka na kulala, wazikuta zishakwenda
Usiombe yakukute
Usiombe kupomoka, toka juu kuja chini
Utajiri kukutoka, kufata umasikini
Twaweza tukakuzika, usipokuwa makini
Usiombe yakukute.
Nakoma ninatoweka, yalikuwa ni maoni
Mekosa cha kuandika, hiki hiki chukueni
Nimechoka nyaka nyaka, natulia kivulini
Nawatakia siku njema.

COMMENTS