Swala ya tarawehe

SWALA YA TARAWEHE Tarawee ni nini?   Swala ya Tarawee ni Swala ya jamaa ambayo Waislamu huswali ndani ya Mwezi wa Ramadhani. Neno...





SWALA YA TARAWEHE


Tarawee ni nini?
 
Swala ya Tarawee ni Swala ya jamaa ambayo Waislamu huswali ndani ya Mwezi wa Ramadhani. Neno ‘tarawee’ linatokana na mzizi wenye sehemu tatu raa.waa.haa, unaoweza kuwakilishwa na herufi r.w.h za Kiswahili. Neno rahah la Kiarabu (mapumziko) linatokana na mzizi huu.
Tarweehah ni pumzimko moja mahususi si mapumziko ya moja kwa moja. Taraweeh ni wingi wa tarweeha. Hivyo, Kilugha, Swala ya Tarawee, Salat at-Taraawee, maana yake ni “Swala ya Mapumziko”.
Jina la swala hii limetokana na mtindo wa Maswahaba ambao walikuwa wakikaa vikao vya mapumziko baada ya kila rakaa nne au duru za Swala, wakiziswali kwa mfululizo wa rakaa mbilimbili kama ilivyoelezwa na Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, akimwambia Bedui mmoja aliyeuliza kuhusu Swala za Nawafil za usiku, imenukuliwa katika Bukhari na Muslim.
Mbali ya kufanya hivyo katika swala ya tarawee, pia tunajifunza kuwa ni jambo la kiafya kuwa wakati tunapofanya kazi au ibada, tuwe na mapumziko kidogo ya hapa na pale.


2. Ni nini Hukumu ya Kisheria juu ya Swala ya Tarawee?
Swala ya tarawee ni sunna mu̢۪akkadah (sunna iliyokokotezwa) kwa wanaume na wanawake. Inapendekezwa kuwa, swala hii iswaliwe kwa jamaa Msikitini. Kama mtu hawezi kuswalia Msikitini, basi aswali kwa kuunga jamaa na watu wa nyumbani kwake.
Aidha inapendekezwa kuwa Imamu atulie kwa mapumziko mafupi kila baada ya rakaa nne kama walivyofanya Maswahaba. Wakati wa mapumziko ni vizuri kwa wale wote wanaoswali kukaa kitako na kutaamuli (kuzama katika tafakuri juu ya MwenyeziMungu) kimyakimya au kumdhukuru  MwenyeziMungu kwa matamshi. Imamu ajitahidi kumaliza Qur’an yote angalau mara moja tu katika Swala ya Tarawee ya Ramadhani nzima.


3. Je Swala ya Tarawee Ilisimamishwaje Wakati wa Mtume na Maswahaba?
Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, aliisimamisha Swala ya Tarawee kwa vitendo. Aisha kasimuliwa kuwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, aliingia Msikitini katika mzamo wa usiku (mwezi wa Ramadhani) na akawaongoza baadhi ya Maswahaba katika Swala. Alfajiri yake watu wakajadili kile alichofanya Mtume, swallallahun alayhi wa sallam, na usiku uliofuata watu wengine zaidi ya wale wa jana yake wakaswali pamoja na Mtume, swallallahu alayhi wa sallam. Usiku wa tatu, watu wakaongezeka zaidi, na usiku wa nne, Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, hakuja Msikitini hadi pale ilipofika Swala ya Alfajir. Alipomaliza kuswali Swala ya Alfajiri, akawaelekea watu na kutamka shahada (kama utangulizi) na kusema: “Ama baada ya hayo: Sikujua kama mlikuwa mnanisubiri nifike, lakini nilichelea kuwa (Swala ya Tarawee) ingeweza kufaradhika kwenu nanyi msingeweza (kuitekeleza faradhi hii).”
Baada ya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, kutawafu, hofu ya tarawee kuwa faradhi ikatoweka. Kwa hiyo, hapakuwa na ubaya kuiswali rasmi swala ya Tarawee Msikitini. Ndipo Umar Ibn Al-Khattab alipowaamuru Maswahaba kuswali Tarawee kwa jamaa Mwezi wa Ramadhani, nao wote wakaridhia. Hatua hii ya Umar ilizingatia kile alichofanya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, na hivyo, haikuwa bidaa. Uhalali wa Swala ya Tarawee ukathibitishwa zaidi na Maafikiano ya Maswahaba.


4. Ni Upi Uhusiano Kati ya Swala ya Tarawee na Qiyam al-Layl (Kisimamo cha Usiku)?
Kwa uhalisia wake, Swala ya Tarawee ni aina ya Qiyam al-layl (kisimamo cha usiku). Kwa hiyo, kwa mtazamo wa ki-fiqh, Swala ya Tarawee na Qiyam al-layl ni sawa tu. Tofauti iliyopo baina yao sanasana ni ya maana tu ya maneno kutokana na ukweli kuwa Swala ya Tarawee ni Qiyam al-layl mahususi ambacho huswaliwa kwa jamaa ndani ya mwezi wa Ramadhani, mara nyingi muda mfupi baada ya Swala ya Isha.


5. Je Swala ya Tarawee ina Rakaa ngapi?
Kwa kuzingatia ukweli kuwa Swala ya Taraweh ni nawafil tu, hakuna tofauti miongoni mwa wanazuoni kuwa swala hii inaweza kuwa na idadi yoyote ya Rakaa. Hata hivyo, licha ya maafikiano hayo ya wanazuoni, idadi ya rakaa za tarawee, wakati mwingine, imekuwa sababu ya khitilafu hasa baina ya makundi fulani ya Waislamu.
Zipo sababu kuu mbili za hali hiyo:

  1. Ukosefu wa elimu ya jambo hilo
  2. Hadith iliyosimuliwa na Aisha (radhiAllahu anha) kuwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, kamwe hakuzidisha rakaa 11 za Swala za Usiku, ama iwe Ramadhani au mwezi mwingine (Bukhari na Muslim).
Kuhusiana na sababu ya kwanza, tiba inaweza kupatikana kirahisi tu kwa kuwaelimisha watu juu ya hukumu inayohusu Swala ya Tarawee. Kuielewa vibaya Hadith hiyo, kumewapelekea baadhi ya watu kudhani kuwa rakaa 11 ndiyo kikomo, inayozidi ni bidaa, na hivyo, ni batili.
Dalili kuwa tarawee inaweza kuwa na idadi yoyote ya Rakaa ni kama ifuatavyo:
  1. Maswahaba waliswali tarawee kwa rakaa 21 (Taz. Sahih, Muwatta), pia waliswali rakaa 23 (Taz. Sahih, Na.3270, Al-Bayhaqi, As-Sunan Al-Kubraa) na kulikuwa na maafikiano miongoni mwao kuwa jambo hili linaswihi. 
  2. Umar ibn Abd-Aziz (maarufu kama Khalifa wa Tano) yeye alikuwa akiswali swala ya Tarawee rakaa 39. 
  3. Katika Hadith iliyotajwa hapo juu, Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, alimwambia Bedui aliyemuuliza namna gani iswaliwe swala ya usiku, kuwa ni “mbili- mbili..tu” bila kuweka kikomo (Bukhari na Muslim). Sana sana alichokisema mwanazuoni yeyote yule ni idadi tu iliyopendelewa. 
  4. Sehemu kubwa ya umma ikiwa ni pamoja n a Maimamu wa Madh-hab nne za Fiqh-inakubali kuwa hakuna kikomo katika idadi ya Swala za Nawafil, ndani ya muda wake unaoruhusiwa. Tarawee nayo pia ni Swala ya Nawafil. 
  5. Hadith iliyotajwa hapo juu inasema kuwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, kamwe “hakuvuka” rakaa 11 katika Swala za Nawafil Usiku. Bila shaka hii inajumuisha ile ambayo tunaiita Swala ya tarawee, au qiyam al-layl.
Sasa basi, kama mtu anasema kuwa inakatazwa kuswali zaidi ya Rakaa 11, basi yeyote yule aliyeswali tarawee asingeliweza tena kuswali nyumbani peke yake hata wakati wa Laylatul Qadr, au wakati wowote ule-na ubatili wa rai hii uko wazi kabisa. Kwani wakati ipo matini inayotaja idadi ya rakaa alizoswali Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, hakuna matini yoyote inayoweka kikomo chake.
f. Ni dhambi kupawekea mipaka migumu pale ambapo MwenyeziMungu ameacha nafasi huru kwa ajili ya watu. Kwa baadhi ya watu ni rahisi zaidi kwao kuswali rakaa nyingi fupifupi, na kwa wengine, ni mapendeleo yao kuswali idadi ndogo ya rakaa lakini kwa kisimamo kirefu.


6. Ni zipi Fadhila za Swala ya Tarawee?
Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema: “Swala bora baada ya Swala ya Faradhi ni ile ya Usiku.” (Muslim). Pia amesema: “Yule anayesimama (kwa ajili ya qiyam al-layl) katika mwezi wa Ramadhani-kwa imani na kwa kutafuta fadhila za MwenyeziMungu-huyo atasamehewa dhambi zake zote za nyuma.”
Yatupasa kuichukua hiyo kama ni ukumbusho na motisha kubwa ya kuutumia vema mwezi mtukufu wa Ramadhani na tudumu na Swala ya Tarawee mwezi mzima ili tutoke katika mwezi huu tukiwa wasafi wa moyo na watupu wa dhambi InshaAllah. 



 Imenakiliwa na sayyidbunduki.blogspot.com


 

COMMENTS

 


 


TANGAZO TANGAZO

TANGAZO  TANGAZO

Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,7,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: Swala ya tarawehe
Swala ya tarawehe
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjRWOHz9naxKctCtenJYh3OfkRFBwMiwXmaANwGIlGC2XO2O9IxzOtzU5kOgcjohHBKfp51lXNz8YyZ-q5TvLXXeO1YhJbM0ZyTk8_fMsujndJSpO2y71YTtn4-Cnd_zUhCy3my8_3Xvrw/s400/Ramadan+Kareem.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjRWOHz9naxKctCtenJYh3OfkRFBwMiwXmaANwGIlGC2XO2O9IxzOtzU5kOgcjohHBKfp51lXNz8YyZ-q5TvLXXeO1YhJbM0ZyTk8_fMsujndJSpO2y71YTtn4-Cnd_zUhCy3my8_3Xvrw/s72-c/Ramadan+Kareem.jpg
mrbunduki
https://sayyidbunduki.blogspot.com/2018/05/swala-ya-tarawehe.html
https://sayyidbunduki.blogspot.com/
https://sayyidbunduki.blogspot.com/
https://sayyidbunduki.blogspot.com/2018/05/swala-ya-tarawehe.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content