Yamevunja wangu wigo, ni mtupu ndugu yenu
Matatu haya mapigo, sitosahau mwenzenu
Kama nimetwishwa gogo, sina m badala mbinu
NAWAKUMBUKA DAIMA, NDUGU HAWA ABADANI
Kuwataja sina budi, majina nimekariri
Wa kwanza ni MOHAMEDI, baba
yake ni Bakari
Rafiki mwenye weledi, katangulia kaburi
NAWAKUMBUKA DAIMA, NDUGU HAWA ABADANI
Mudi ninamkumbuka, kwa nzuri zake sifa
Awali nilipofika, Shamsil maarifa
Nilikuwa wake nyoka, kweli Mudi amekufa?
Machozi yananilemga, nashindwa kujizuia
Mungu akuweke pema, sina zaidi ya haya
Nimeshindwa la kusema, ingawaje nimepwaya
Nakuombea salama, na nduguzo wa KWABAYA
NAWAKUMBUKA DAIMA, NDUGU HAWA ABADANI
Pili tawatajieni, leo hii si tumoro
Ni ndugu yangu HOSENI, mtoto wa samtoro
Mkalamo ya handeni, umetuacha kihoro
Bunduki akulilia, umemuacha na nani?
Ninashindwa kunyamaa, hata beti nikatunga
Mwaya huenda asaa, chozi langu likafunga
Nakuombea duaa, Adhabu atakukinga
Bunduki akulilia, umemuacha na nani?
Yananijaa majonzi, pweke nimeelemewa
Nakumbuka zile enzi, tulipokuwa MAAWA
Nakumbuka yako kazi, Qur ani na daawa
Bunduki akulilia, umemuacha na nani?
Kinywa wazi natamka, wasomaji waelewe
Kimwili umenitoka, kiroho niko na wewe
Ishallaah tutaongoka, nasisi tusamehewe
Bunduki akulilia, umemuacha na nani?
Wa tatu mudiri wangu, kwa leo nafunga dimba
Huyu ni mwalimu wangu, UMMARI bin MAHAMBA
Na pia mlezi wangu, jueni hivyo ya kwamba
Ameacha mtihani, bado sijautatua
Kijiji cha mkalamo, ameacha pengo kubwa
Lililo tuzidi kimo, na bado halijazibwa
Kijiji ni mzizimo, si wadogo si wakubwa
Ameacha mtihani, bado sijautatua
Nashindwa niseme nini, shekhe kumuelezea
Nabaki inama chini, nazidi kujililia
Ametuacha na nani, elimu imepotea
Ameacha mtihani bado sijautatua
Amenipa mtihani, siijui yake njia
Je ni mtihani gani?, siku nitaja kwambia
Leo yupo kaburini, Allah amemchukua
Ameacha mtihani, bado sijautatua
Mzee hakuni khini, mengi kanisaidia
Hata nilipotamani, na ndoa kuiingia
Yeye ndo kanidhamini, na ndiye kaniposea
Ameacha mtihani, bado sijautatua
Namwomba aliye juu, Mwenyezi mungu Jalali
Daraja zilizo juu, amweke kwa kila hali
Hawajui wajukuu, nilopata kiukweli
Ameacha mtihani, bado sijautatua
#usiombe kuondokewa na unayemtegemea.
Shairi
limeandikwa
Tar 31.07.2018 siku ya jumanne saa 1.30 usiku.

COMMENTS