Tulia e moyo wangu, mtambue Mola wako
Usifwate walimwengu, wakupelekako siko
Fuata mambo ya Mungu, kesho pepo iwe yako
NAIUSIA NASI YANGU -
Dunia hii twavuka, wengi tulikuwa nao
Machoni wametutoka, kuenda kwa Mola wao
Leo una hadaika, waovu achana nao
NAIUSIA NAFSI YANGU -
Imepambwa pambo feki, ili sisi tupotee
Tuende bila breki, mwishowe tutokomee
Ni mfano wa handaki, inauma aisee
NAIUSIA NAFSI YANGU -
Usifwate walimwengu, wakupelekako siko
Fuata mambo ya Mungu, kesho pepo iwe yako
NAIUSIA NASI YANGU -
Dunia hii twavuka, wengi tulikuwa nao
Machoni wametutoka, kuenda kwa Mola wao
Leo una hadaika, waovu achana nao
NAIUSIA NAFSI YANGU -
Imepambwa pambo feki, ili sisi tupotee
Tuende bila breki, mwishowe tutokomee
Ni mfano wa handaki, inauma aisee
NAIUSIA NAFSI YANGU -
Maisha mafupi sana, zaidi ya mbili kimo
Ni usiku na mchana, au kidogo kipimo
Shikilia ya Rabana, nakuvika hili somo
NAIUSIA NAFSI YANGU -
Mfano huu kariri, hwenda mwisho ukatii
Unaemwona mzuri, si huoni husikii
Hakuumbwa kwa uturi, bali tone la manii!!
BINAADAMU HANA THAMANI -
Ewe moyo tulizana, leo ninakukumbusha
Penye kheri shikamana, yajayo yafurahisha
Ukiona sina mana, yajayo yasikitisha
UKIONA NI MZAHA - Utakuja jionea
Tumeitwa uma bora, kwasabu twausiana
Penye kheri na hasara, lazima kuzinduana
Ama kama nakukera, UTAPATA TABU SANA
NAIUSIA NAFSI YANGU - pamoja na kuwausia ndugu zangu

COMMENTS