Moyo wangu unanini, mbona unalia sana
Umenitia huzuni, toka nilipokuona
Alokuudhi ninani, nakuomba hebu nena
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI
Alokuudhi ninani, nakuomba hebu nena
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI
Moyo nieleza kisa, kilokutia uchungu
Usinifiche kabisa, nakuomba moyo wangu
Lipi linalokutesa, na kukutia tewengu?
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI
Usinifiche kabisa, nakuomba moyo wangu
Lipi linalokutesa, na kukutia tewengu?
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI
Moyo chukua kalamu, kiwa huwezi kusema
Moyo usinidhulumu, ukanitia na homa
Na mwenzio nina pumu, hunionei huruma
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI.
Moyo usinidhulumu, ukanitia na homa
Na mwenzio nina pumu, hunionei huruma
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI.
Moyo punguza kulia, kilio sijambo jema
Moyo wangu niambia, lipi linalokuchoma
Ukilia nitalia, siwezi kukutazama
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI.
Moyo wangu niambia, lipi linalokuchoma
Ukilia nitalia, siwezi kukutazama
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI.
Moyo punguza hasira, niambie unanini
Zituze zako fikira, uneleze kwa makini
Mbona leo umefura, kwani kuna shida gani?
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI.
Zituze zako fikira, uneleze kwa makini
Mbona leo umefura, kwani kuna shida gani?
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI.
Moyo usisikitike, nena wala usijere
Yanene yafahamike, usinichezee shere
Tujue wapi tushike, ama kabisa tugure
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI.
Yanene yafahamike, usinichezee shere
Tujue wapi tushike, ama kabisa tugure
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI.
Moyo punguza ghadhabu, asikughuri shetwani
Moyo naomba jawabu, walizwa na jambo gani
Nena kwa ustarabu, nipo mwako miguuni
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI.
Moyo naomba jawabu, walizwa na jambo gani
Nena kwa ustarabu, nipo mwako miguuni
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI.
Moyo wangu vumilia, bado tumo baharini
Moyo asiyekujua, hawezi kukuthamini
Iko siku nakwambia, nasi tutapata pwani
SILIE MOYO WAUNGU, UTANILIZA NA MIMI.
Moyo asiyekujua, hawezi kukuthamini
Iko siku nakwambia, nasi tutapata pwani
SILIE MOYO WAUNGU, UTANILIZA NA MIMI.
Moyo usifanye pupa, tulia uwe makini
Usiwaogope papa, pamabana ujiamini
Sisi leo tuko hapa, kesho tuko bandarini
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI.
Usiwaogope papa, pamabana ujiamini
Sisi leo tuko hapa, kesho tuko bandarini
USILIE MOYO WANGU, UTANILIZA NA MIMI.
Moyo mwisho nakukanya, ya waja usisikie
Moyo tena nakuonya, bure usilielie
Na yote walonifanya, wewe yasikusumbue
USILIE MOYO WANGU,UTANILIZA NA MIMI.
Moyo tena nakuonya, bure usilielie
Na yote walonifanya, wewe yasikusumbue
USILIE MOYO WANGU,UTANILIZA NA MIMI.

COMMENTS