IMEANDALIWA NA KUANDIKWA
NA:-
"bunduki.com"
Katika harakati za
maisha ya kila siku ni lazima zitatokea siku ambazo zitabaki kuwa historia. Hii
ni kutokana na jinsi ambavyo maisha huenda na kuendelea.
Hivyo basi;-
Bunduki.com leo inakuletea historia
maalum ya safari ya kutoka Mbeya kuelekea Iringa kwa ajili ya matembezi
yalioambatana na kuwaona ndugu zangu ambao nilikuwa nao Mbeya kwa muda mrefu
lakini kwa muda huu walikuwa wamehamishiwa huko Iringa. Hawa mabwana ni bwana
Omy Krish pamoja na kijana wake Omari Saidi Alamtara. Kutokana na ratiba za
kazi ilinibidi kuondoka siku ya jumamosi jioni ili nisiweze kukosekana ofisini
siku zote za wiki.
Nilianza safari siku ya
jumamosi jioni baada ya kufunga Ofisi, majira ya saa 12 jioni. Hii ilikuwa ni
siku ya Tarehe 30 / 03 / 2019. Niliondoka Mbeya mjini kwa usafiri wa pikipiki
(boda boda) kuelekea mji mdogo wa Uyole ambapo kwa muda huo nilitarajia kupata
magari yaendayo Dar ili nishukie Iringa.
Kutokana na sababu
ambazo zilikuwa nje ya uwezo wangu, nilikosa gari za kuelekea Dar, na hatimaye
nilipata mabasi madogo (coaster) yaendayo Njombe. Hivyo nilipaswa kushuka
Makambako na kutafuta gari nyingine ambazo zinafika Iringa kwa namna moja au
nyingine. Gari ile (Coaster) iliondoka pale Uyole mnamo majira ya saa moja
hivi. Mwendo wa takriban masaa manne tuliweza kufika Makambako na kushuka pale.
Nililazimika kusimama njiani ili niweze kupata gari yoyote nipande kuelekea
Iringa hata kama ingekuwa ni gari ya mizigo. Basi nikatoa kamera yangu kwenye
begi na kujipiga picha mbili tatu.
Twende sawa
Hapa ni mji wa Makambako nikiwa nimesimama barabarani kusubiri usafiri wa Iringa (Picha na mimi mwenyewe).
|
Muda ule ulikuwa tayari
ni usiku hivyo kwa magari mengi haikuwa rahisi kusimama kwa sababu mbalimbali
za kiusalama. Lakini baada ya dakika takriban 40 nilibahatika kupata gari kubwa
aina ya scania, ambayo sikujua kwa haraka haraka ilikuwa na mzigo gani lakini
walinikubalia na kunichukua. Tulisafiri kwa raha na salama mpaka kufika katika
mji wa Iringa ambapo wenyeji wangu walikuwa wananisubiria kwa hamu.
Nilipokaribia niliwafahamisha kwa simu ya mkononi na walianza kusogea
barabarani. Nilifika Iringa majira ya saa 7 na dakika nyingi sana usiku.
|
Nilimshukuru Mungu kwa
kufika salama salmini, na tukapitia mgahawani kupata chai. Na hali ilikuwa kama
hivi
Hapa ni Mgahawani tulipoingia kwa ajili ya kupata chai safi kabisa (Picha na Omy Krish)
|
Baada ya hapo tulielekea
nyumbani na kupumzika kwa ajili ya kujiandaa na majukumu ya siku iliyofuata
ambayo ilikuwa ni jumapili tulivu kabisaa. Baada ya kumaliza majuku ya hapa na pale
Mwenyeji wangu bwana Omy Krish (Chuga) aliamua kutupeleka na kututembeza sehemu
tofauti tofauti za mji wa Iringa ikiwemo katika Ofisi ya UNIQUE PRINTING
SOLUTION ambayo ilifunguliwa kule. Pamoja na Omari wale wawili laikini pia
alikuweko kijana mwingine kwa wakati ule ambaye anaitwa Abdul
![]() |
Hapa ni nyumbani na huyu bwana ni mwarabu akiwa ameweka pozi matata. |
Asubuhi kulipopambazuka ilikuwa ni siku ya kutekeleza majukumu ambayo yalinipeleka kule. Hivyo baada ya kujiandaa na kupata chai nzito ya asubuhi, tulitoka pamoja na familia yote kuelekea ofisini kwa hawa mabwana ili kuendelea na michakato yetu.
Nikaona ni fursa njema ya kushea nawe picha za mji ule wa Iringa kama ambavyo utauona hapo chini.
Baadhi ya maeneo ya mji wa Iringa (pcha na bunduki.com) |
Bunduki.com akiwa na kijana ABDUL (picha na Omy Krish) |
bunduki.com akiwa UNIQUE PRINTING SOLUTION (picha na mwarabu) |
Baada ya kuzunguka mjini
kwa muda mrefu, Mwenyeji wetu aliona ni bora kutupeleka katika moja ya maeneo
ya kihistoria ambapo hujulikana kama GANGILONGA. Sehemu ambayo kuna jiwe ambalo
linahistoria kubwa katika Mkoa wa Iringa. Msafara wetu ulikuwa kama hivi.
Msafara ulikuwa na jumla ya watu takriban 6, lakini kutokana na kulinda
maadili watu wengine hamtawaona katika picha.
Twende sawa
Vijana wakiwa katika safari ya kuelekea Gangilonga - Kutoka kulia ni Abdul, Omari mwarabu na Omy Krish (picha na buunduki.com) |
Kwambali unaonekana mji wa Iringa baada ya kuuacha kilomita kadhaa. |
Kiongozi wa msafara Omy Krish, akiwa katika harakati za ku record matukio muhimu. |
Abdul akirekodi matukio |
Gangilonga |
Omy krish (kushoto) akifanyiwa mahojiano na mwandishi wetu. |
Abdul |
The chuga Kabadishaa |
Baada ya kumaliza zoezi lile ulikuwa ni muda muafaka sasa wa kurudi nyumbani kwani hata hivyo njaa zilianza kuuma. Kiongozi wa msafara aliamuru watu warudi nyumbani. Lakini kabla ya kufika nyumbani tulipitia hotelini na kupata chakula kitamu zaidi. Zifuatazo ni picha ambazo zilipigwa nje ya hoteli hiyo ya kisasa.
Twende sawa
Baada ya kumaliza mambo yote muda ulikuwa umeshasonga sana kwani nilitakiwa kurudi Mbeya siku ile ile na Jumatatu niwe kazini kwa uwezo wa Allaah. Tulirudi nyumbani na kujiandaa kwa ajili ya safari. Ndugu zangu walinipeleka mpaka stand ya mabasi na kukata tiketi katika basi la Hajis ambalo hutoka Arusha kuelekea Mbeya.
![]() |
Hapa ni stand ya mabasi Iringa. Zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya kuondoka. |
Baada ya takriban dakika kumi na tano gari ilifika na nikaanza safari. Hii ilikuwa ni majira ya saa kumi na moja na dakika kadhaa jioni. Nilifika Mbeya salama kabisa mnamo saa 5 usiku.
Na huu ndio mwisho wa muhtasari huu wa safari ya Iringa yenye jina la "IRINGA TOUR" Asante kwa kushiri.
Usisahau ku subscribe hapo chini kwenye blog yetu ili kupata UPDATE nyingine mbali mbali na makala tofauti ambazo zitakuja.
Mwandishi
Saidi R Bunduki.
Ma shaa Allah, safari niya kuvutia kweli
ReplyDelete