IMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA bunduki.com SEHEMU YA PILI Hii ni likizo fupi ya mapumziko ya wiki mbili ambayo niliipata kwa viongo...
IMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA bunduki.com
SEHEMU YA PILI
Hii ni likizo fupi ya mapumziko ya wiki mbili ambayo
niliipata kwa viongozi wangu wa kazi. Nayo ilikuwa ni baada ya sikukuu ya Iddi
kubwa kuisha (IDD ALHAJJ). Kwakuwa familia yangu walikuwa wameshatangulia
kijijini kwa ajili ya kujumuika pamoja na wazazi, ilinibidi safari ya kwenda
niwe peke yangu.
Tulianza safari rasmi kutoka Mkalamo na kuelekea katika kijiji cha Mkata, ili siku inayofuata
tuanze safari ya kuelekea Arusha na Hatimaye Mbeya. Nikiwa na familia yangu
ambayo ni mke wangu na watoto wangu wawili. Tulianza safari siku ya alhamisi ya tarehe 29 / 08 / 2019. Tuliondoka Mkalamo kwa usafiri wa Basi la Kidato Bus
Service. Tuliondoka Mkalamo majira ya saa tano asubuhi baada ya kusindikizwa na
ndugu na jamaa mpaka stendi. Tulifika Mkata majira ya saa tisa jioni na
kuelekea kwa mwenyeji wetu ambaye ni Ustadh Muhammad Bakari. Huyu bwana ni
mwenyeji wangu wa muda mrefu sana tangu miaka ya 2011. Hivyo ni mara chache
sana ambazo huenda Mkata na nisifike kwake na ni kwasababu maalum.
Tulikaa pale siku ile yote ili kusubiri siku ifuatayo na
kuanza safari.
Kulingana na majukumu ya kikazi, niliataka familia yangu
wao watangulie Mbeya kwa kupitia katika kijiji cha Ruvu ambako yuko dada yetu na kulala huko nami niende kuendelea na majukumu ya Kampuni na hatimae
tukutane Mbeya. Hivo basi ilibidi siku ifuatayo wao waanze safari kuelekea Ruvu
kwa dada Sofia nami nilianza safari ya kuelekea Arusha. Wakati nikielekea stendi nilikutana na vijana wangu ambao walikuwa wanakwenda masomoni Madrasa Dar es Salaam. Nikaona itapendeza kama nikipata nao walau picha (selfie)
![]() |
| Picha (kutoka nyuma) ikimuonesha Ustadh Muhammad akituongoza kuelekea stand. |
![]() |
| Picha ikimuonesha Ustadh Muhammad na bunduki.com. Tukiwa katika harakati za kuisafirisha familia |
![]() |
| Nikiwa na baadhi ya vijana wangu ambao walikuwa wanakwenda masomoni (Madrasa) Dar es Salaaam |
Nilianza safari majira ya saa nne na nusu pale Mkata
nikiwa na basi la "CHAKITO" ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam. nilifika majira ya saa moja usiku.
Nilimsubiri ndugu yangu bwana Omy Krish ambaye yeye kwa siku ile alikuwa
anatoka Mbeya kuja Arusha ambapo wote tulifika nyumbani kwao kwa Ustadh Hashim
ambaye ni moja ya viongozi wakubwa wa Kampuni yetu ya Galaxy Computers. Bwana Omy krish alipokaribia kufika nilisogea maeneo ya stendi na kuweza kuelekea nyumbani pamoja. Kulipopambazuka asubuhi tulijiandaa na kuelekea HQ (MAKAO MAKUU) kwa ajili ya kukutana na kuianza safari ya kuelekea Kisongo kwa ajili ya semina.
| Nikiwa na kiongozi HASHIM nje ya nyumba yake muda mchache kabla ya kuondoka. (Picha na Omy Krishna) |
| Omy krish kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika semina (Picha na bunduki.com) |
Siku ya jumamosi, tarehe 31 / 08 / 2019 ndio ilikuwa siku
rasmi ya Kikao ambacho tuliitwa kwacho. Kikao / Semina ile ilifanyika maeneo ya KISONGO ambako ni kama
kilomita 30 kutoka Arusha mjini.
| Omy Krish akitoa maelezo mafupi kwa waandishi wetu kuhusiana na semina hiyo elekezi (Picha na bunduki.com) |
| Katika ukumbi rasmi wa Mkutano wa Galaxy katika shule ya sekondari ya Assalafi islamic Kutoka kushoto ni Iyaka, Omy Krish, Bunduki.com, Kombo, Mohamed pamoja na Kasim (Picha na mpigapicha wetu) Omy Krish akiwa na Ally Mote nje ya ukumbi wa Mkutano wakizungumza jambo (Picha na bunduki.com) |
| Muda wa chai - Omy krish (kulia) akiwa na bunduki (Picha na Mohamed Iyyaka) |
Semina yetu ilimalizika mnamo majira ya saa kumi jioni, baada ya hapo tuliamuriwa kuelekea makao makuu ambapo ni Arusha mjini kwa ajili ya mafunzo mengine ya muda mfupi.
| Picha ambayo haina ubora sana ikimuonesha Omy krish akiwa maeneo ya Godown Galaxy computers (HQ) |
| Kasimu akielendelea na kuwaellimisha wafanyakazi wa Galaxy kuhusu baadhi ya spea za toner cartridge (Picha na bunduki.com) |
| Bwana Kasim akitoa darasa juu ya baadhi ya toner cartridge. (Picha na Bunduki.com) |
Baada ya kupata mafunzo mafupi pale godown HQ, kiongozi wetu Sheikh Mubaraka aliamuru watu waelekee maeneo ya Ofisi mpya za Galaxy computers tawi la Arusha kumalizia shughuli za mwisho mwisho na kuweza kuondoka.
ZIFUATAZO ni picha zikionesha ofisi mpya ha Galaxi Arusha na baadhi ya wafanyakazi wakifurahia uwepo wao hapo
| Kutoka kulia nia Kasim, Abuu na Omy krish. |
| Bunnduki.com akiwa na Kasim |
| Bunduki.com kulia akiwa na Bwana Bakari - wakiwa na furaha iliyo taradadi. |
| Baadhi ya wafanyakazi wa Galaaxy wakiwa nje ya ofisi. |
Baada ya muda tuliruhusiwa na kwenda kupumzika kwani mpaka hapo tayari ilikuwa ni saa moja kama na nusu usiku.
Siku iliofuata ilikuwa ni jumapili, ingetakiwa siku ile
turudi Mbeya lakini haikuwezekana kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo
wetu. Hivyo siku ile tuliitumia kwa ajili ya kutembea maeneo tofauti tofauti ya
Jiji la Arusha.
Utakutana na vijana mashuhuri na machachari waliozaliwa na kukulia Arusha wakiongozwa na BRIGEDIER DONLEY GUCKY(OGOPA SANA)
Utakutana na vijana mashuhuri na machachari waliozaliwa na kukulia Arusha wakiongozwa na BRIGEDIER DONLEY GUCKY(OGOPA SANA)
Kwa leo tuishie hapa katika sehemu hii ya pili ya likizo yangu.
Tafadhali usikje ukakosa sehemu ya tatu na ya mwisho ambapo bado tukiwa ndani ya jiji la Arusha (CHUGGA) na viunga vyake.
Shukrani za dhati ziwaendee wote walioshiriki katika kuhakikisha jambo hili linafanikiwa kwa namna moja ama nyingine.



haya baba naona mambo yapo tununu kabisaa
ReplyDeletekama kawaaaaaaaaa
Delete