Kila mwaka katika kampuni yetu ya Galaxy computers hua tunakuwa na semina ya kufunga mwaka ambayo hukutana wafanyakazi wote kujadili mambo mbali mbali yanayohusiana na biashara kwa ujumla. Ikiwemo Mafanikio, changamoto, Mpangokazi n.k.
Kwa mwaka huu semina ilipangwa kufanyika katika jiji la Arusha, ambapo ndio makao makuu yetu ya Kampuni.
Yafuatayo ni maelezo ya ziara yangu fupi kutoka Mbeya kuelekea Arusha. Lakini pia katika kipindi kifuatacho nitakuletea mtiririko mzima wa matukio mbali mbali kutoka Arusha nikiwa na ndugu zangu na jamaa zangu katika pirika pirika za huko. Kubwa katika hilo nitakuletea tukio zima la kutembelea moja kati ya sehemu za ki historia huko Mkoani Arusha.
Usisite kuwa nasi katika mitandao yetu ya kijamii kama facebook, twitter, instagram na youtube channel yetu.
TWENDE SASA !!!
Niliondoka Mbeya siku ya tarehe 24 / 12 / 2019 hii ilikuwa ni siku ya Jumanne. Nilisafiri na basi la Kampuni ya Arusha Express. Gari iliondoka majira ya saa 11:55 asubuhi (alfajiri)
Tulipofika makambako gari ilionekana kuzidi uzito katika mizani na dereva kutakiwa kulipa ushuru. Dereva hakuwa muelewa na kutotaka kukubaliana na hali halisi. Ilitubidi kuzuiwa pale kwa muda mrefu mpaka abiria walipoamua kuandamana kuelekea katika ofisi husika.
 |
Baadhi ya abiria wakiwa chini kusubiri muafaka |
 |
"bunduki.com" katika harakati za kusubiri muafaka wa safari |
 |
Abiria wakielekea ofisi ya mizani, ili kuzungumza na viongozi. |
 |
Abiria wakisikiliza kwa makini malezezo yaliyokuwa yakitolewa na Mmoja ya viongozi wa mizani |
Baada ya takriban saa moja na nusu muafaka ulipatikana na abiria kuweza kuendelea na safari.
Kwakuwa pale tulichukua mda mwingi kiasi, Tulifika Arusha majira ya saa 6:10 usiku badala ya kufika saa 4 kama tulivokuwa tunakusudia.
Nilishukia katika stendi ya Majengo ya chini ambako ni karibu na walipo wenyeji wangu Ambao ni Ustadh Hashim akiambatana na Omy Krish baba la baba.
Siku ya pili ilikuwa ni siku ya Semina ambayo ilitupeleka kule. semina ya mwaka huu ilikuwa ikifanyika katika mji wa Kisongo nje kidogo ya JIJI la Arusha. Tuliondoka nyumbani majira ya saa moja asubuhi ili kutokea barabarani ili kusubiri usafiri wa Kampuni.
 |
Omyi Krish baba la baba, akimpiga picha kwa mbaali kiongozi wetu Hashim wakati anatoka nyumbani. |
 |
Nje ya Jengo la AIM MALL ilipo barabara ya kuelekea Kisongo. Hapa ni wakati wa kusubiri usafiri |
Baada ya dakika takriban kumi na tano gari ilifika na tuliekea sehemu ya tukio.
Semina ile ilifanyika kwa muda wa siku mbili yaani jumatano na alhamisi za tarehe 25 na 26 mwezi wa 12 mwaka wa 2019.
Zifuatazo ni baadhi ya picha katika semina ile;-
 |
Picha hizo ni Baadhi ya wadau wakifuatlia kwa makini somo ambalo lilikua likitolewa na Kiongozi |
 |
Saidi Bunduki akiwasilisha ripoti kutoka Mbeya |
 |
Kombo Ali kutoka Tanga akiwasilisha ripoti yake kutoka Tanga |
 |
Omyi Krish akiwa na Kibabedi wakizungumza jambo baada ya kutoka kwenye simna |
 |
Baba la baba |
 |
Omy Krish akiwa na Kiongozi Kasim kutoka katika kitengo cha PRODUCTION |
Semina ile ilimalizika salama kabisa na siku zilizofuata kulikuwa na Tour / safari maalum za kutembelea vivutio mbali mbali vya watalii.
Usikose sehemu ya pili na ya tatu ya Arusha Tour ili kujionea matukio tofauti tofauti.
Imeandaliwa na "bunduki.com"
Chini ya udhamini wa;-
GREEN TEST
Wauzaji na wasambazaji wa juisi ya matunda JIJINI Arusha
ASANTE KWA WOTE WALIOSHIRIKI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE
COMMENTS