Hapa tutazungumzia - WATER FALLS TOUR (A) Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya watalii. Miongoni mwake ni mbuga za wanyama, Ml...
Hapa tutazungumzia - WATER FALLS TOUR (A)
Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya watalii. Miongoni mwake ni mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro, Maziwa makubwa pamoja na vitu vingi. Arusha ni miongoni mwa mikoa ambayo imebarikiwa pia vovutio vingi pia. na tunapozungumzia watalii wapo watalii wa ndani ambao ni sisi wenyewe kwanza kisha ni wageni kutoka nchi za nje.
Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya watalii. Miongoni mwake ni mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro, Maziwa makubwa pamoja na vitu vingi. Arusha ni miongoni mwa mikoa ambayo imebarikiwa pia vovutio vingi pia. na tunapozungumzia watalii wapo watalii wa ndani ambao ni sisi wenyewe kwanza kisha ni wageni kutoka nchi za nje.
Baada ya kupata fursa ya kupumzika, sisi kama crue ya "bunduki.com" yenye watu sita tuliamua kutembelea eneo la WATER FALLS lililoko kando kando ya Mlima Meru ambao hupatikana Arusha.
Hapa tunakuletea tukio zima kwa ujumla wake ili kushea nawewe yale ambayo tulipitia mpaka kufanikiwa kufika katika eneo hilo pamoja na ugumu wake. Safari hii ilikuwa ni ya watu 6 ambao ni Omari Ntisi (Mwongozaji), Omy Krish, Mujahid, Fahad, Victor Chris pamoja nami Saidi Bunduki.
Safari ilianza kwa kuelekea maeneo ya Sanawari, baada ya kufika pale tulipata chakula cha mchana na kisha kuanza safari kamili ya kuelekea huko.
Kutoka kushoto ni Mujide Khan, Donley Gucky, Omy Krish, Victor pamoja na Fahad (Picha na bunduki.com) |
Baada ya kutembea kilomita takriban mbili kuelekea mlimani, tulikutana na kijana mmoja na kumuuliza njia ambayo ungeweza kutufikisha huko. Kijana yule aliyejitambulisha kwa jina moja la FESTO alituelekeza njia mbili, lakini baadaye tuliamua kuchagua njia nzito yenye mlima mkali ili kupasha misuli.
Festo akitoa maelekezo ya kufika sehemu husika |
Vijana wakipokea maelekezo kutoka kwa Kijana Festo. |
Safari inaendelea kwa mwendo kasi |
Wakati Msafara unaendelea nilikutana na vijana wadogo ambao walitamani kupiga picha, niliwafanyia mahojiano mafupi. Moja ya vijana wale alikuwa anaitwa ANNS. Picha zao ni hizi zifuatazo hapa chini.
Vijana wakiwa katika interview maalum na "bunduki.com" |
Picha ya pamoja wadau wakiwa na bwana Festo (mwenye flana nyekundu) mda mchache kabla ya kuagana |
Watu walitembea umbali mrefu sana, takriban masaa mawili yalipita watu wakiwa bado wanapandisha mlima. Vijana walichoka sana na kupumzika. Zifuatazo ni picha zikionesha wadau wakiwa katika mapumziko sehemu tofauti.
Mujide Khan akiwa na Omy Krish, Wakipigwa picha na Donley Gucky |
Victor, Mujide Khan akiwa na Omyi Krish |
Omy Krish akitazama mazingira ya milimani |
Camera man akiwa na Fahad |
Upigaji picha ukiendelea na bunduki.com |
Uchovu umekithiri
Mda mchache kabla ya kuondoka na kuendelea na safari yetu "Picha na bunduki.com" |
Mandhari ya mji wa Arusha ikionekana kutoka juu. |
Vijana wakitazama mandhari ya JIJI la Arusha kutoka juu. |
Baadhi ya wananchi wa jamii ya WAMERU wanaoishi milimani. |
Saidi R Bunduki. (C E O wa Mtandao wa "bunduki.com" |
Baada ya kuumaliza mlima ule mrefu hatimaye tulifika sehemu ya makazi ya watu. Baadhi ya wenyeji tuliwauliza kuhusiana na utaratibu wa kuingia kule. Walituelekeza kuwa ni lazima tuonane na uongozi wa Kijiji. Lakini mpaka muda ule ilikuwa ni takriban saa kumi ya jioni hivyo haikuwa rahisi kuupata Uongozi husika. Na hatimaye tulikutana na bwana mmoja sehemu ya Mapokezi na kutusindikiza mpaka kule. Kutokana na uchovu kukithiri baadhi ya watu ilibidi kupunguza baadhi ya nguo na viatu.
Omy Krish akiwa mbele ya Msafara. |
Bunduki akiwa mbele ya msafara. |
Huyu ni bwana Fahad na Mujahid wakiwa nyuma ya msafara kwa wakati huu. |
Kipengele kifuatacho sasa kilikuwa ni kushuka bonde kuelekea huko maporomokoni. Kiukweli safari hii iligubikwa na changamoto kuu tatu. Ya kwanza ni kupanda mlima, ya pili ilikuwa ni kushuka kwa bonde. Hili ni bonde ambalo lilikuwa na changamoto kubwa sana hasa ukizingatia njia ilikuwa ni nyembamba sana. Na changamoto ya tatu ilikuwa ni baridi kali kule maeneo ya maporokoni.
Hapa katika Sehemu hii tumezungumzia changamoto moja tu ya kupanda mlima. Hebu fuatilia sehemu ya pili kujionea changamoto zilizo wakumba watu katika kushuka mlima na baridi kali huko mtoni mpaka saa za kurudi.
Usisahau kutufollow katika kurasa zetu za kijamii, pia usisahau ku subscribe katika channel yetu ya youtube
Asante
Imeandaliwa na MTANDAO wa "bunduki.com"
Kutazama full video bonyeza link hii hapa chini;-
WASHIRIKI
OMARI NTISI - Muongozaji (Mwenyeji)
OMY KRISH - Director (Kiongozi wa Msafara)
FAHAD (Galaxy man)
MUJAHID (Mujide Khan)
VICTOR CHRISS
SAIDI BUNDUKI (Mwandishi na Kiongozi wa mtandao wa
'bunduki MEDIA'
ASANTE KWA WOTE WALIOSHIRIKI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE
IMEDHAMINIWA NA;-
GREEN TEST
Wauzaji na wasambazaji wa juisi ya matunda JIJINI Arusha
COMMENTS