CORONAVIRUS TIPS
[Zungumza na familia yako]
Kila mmoja ni shahidi juu ya Balaa ambalo kwa sasa dunia nzima inaugua (konora virus - covid 19) Kutokana na hofu iliyotanda kila kona ya dunia kwa sasa kwa watu wa rika zote kuanzia watoto, vijana mpaka wazee. Lakini hofu hii inaweza kuwa kubwa kabisa na ikawa na taswira tofauti kwa watoto wetu kulingana na ukubwa wake. Ukiwa kama mzazi / mlezi ni lazima kulijua hili na kuwa karibu na watoto wako kwa kuwapatia elimu zaidi juu ya hili.
HALI ZOTE HIZI SI SALAMA SANA KWA MTOTO
a. Hofu iliyopitiliza juu ya CORONAVIRUS.
b. Kutokuwa na hfu kabisa.
Unaweza kuuliza kuwa 'Sasa ni Ni vipi tutazungumza na watoto wetu katika hili?'
Kaa nami.
Soma kipande hiki hapa chini.
Kwa watoto ambao wanaonesha kuwa na wasi wasi juu ya hili, mzazi ni lazima kusimamia katika hofu yake na kuhakikisha anakuwa sawa. Mtaalamu mmoja wa Afya ya akili kutoka nchini Marekani alisemwa kuwa "Mtoto wako anaweza kuwa na hofu hata kama hajaiweka wazi kwako" yaani huenda ikawa hajakwambia chochote lakini akawa na hofu juu ya hili. Kwahiyo ni bora wewe mzazi ukafahamu kwa kina suala hili kabla hujaifikisha eliku kwa watoto wako.
MZAZI IELEWE HATARI
Ukiwa kama kiongozi wa familia hakikisha unaelewa vizuri virusi hivi kabla watoto hawajasikia habari zisizo sahihi kutoka kwa wenzao ama kutoka katika vyombo vya habari visivyoaminika na hapo utaweza kujibu maswali yao kwa weledi na ufanisi. Mzazi anatakiwa kuwambia watoto wake kuwa virusi hivi ni virusi vinavyohusiana hasa na mfumo wa upumuaji na pia ni vema kuwafahamisha dalili zake. Unaweza kusoma hapa chini kujua dalili zake kwa kina zaidi.
Dalili za corona
Mzazi anatakiwa kuwaambia watoto wake kuwa wanapaswa kuosha mikono yao kwa muda usiopungua sekunde 15 - 20 pale wanapotaka kula, wanapotoka msalani, pale wanapotaka kwenda kwenye maeneo yenye watu wengi n.k
Bila kusahau kujiepusha na kushika midomo yao, pua na macho.

ZUNGUMZENI
Kama mzazi unatakiwa kusikiliza na kutilia maanani mazungumzo na hofu ya watoto wako na sio kuwakaripia na kuwapuuza, wape umakini na tambua hisia zao.
KWA WATOTO WASIOLITAMBUA KABISA HILI
Hawa ni miongoni mwa watoto wadogo ambao wengi wao bado hawajawa na upambanuzi katika masuala ya kijamii, basi ni vema ukasimamia usafi na umakini wao katika kila hatua ya kazi zao na maisha yao kwa ujumla.
Imeandaliwa na SAIDI BUNDUKI
Lakini kuna mambo 13 ambayo huenda hujayafahamu kuhusu coronavirus-
PITIA HAPA

COMMENTS