Kumuepuka shetani
Nataka ifadhi (Najikinga) kwa Mwenyezimungu kutokana na Sheitwani aliyelaaniwa (Aliyeko mbali na Rehma za Mwenyezimungu)
Bismillahir Rahmaanir Rahiim
(Kwa jina la Mwenyezimungu Mwingi wa rehma mwenye kurehemu)
Katika harakati za kuamrishana MEMA na kukatazana MABAYA, leo nakuja na nukuu fupi juu ya suala zima la kujiepusha na sheitwani katika shughuli na maisha yetu ya kila siku. Nkukumbushe tu ndugu yangu muislamu kuwa mimi sio mjuzi sana wa elimu ya dini,hivyo pale ambapo utakutana na mapungufu basi wasiliana nami haraka kwa kubofya HAPA au unaweza kuweka maoni yako sehemu ya comment
Watu wengi wakisikia habari ya sheitwani moja kwa moja wanafikiri kuwa moja kwa moja ni JINNI, lakini ukweli ni kwamba sheitwani anaweza kuwa mwanadamu au jinni, huyu ni kiumbe ambaye anakushawishi katika kuacha mambo mema na anayekuamrisha katika kufanya mambo maovu. 'Anaamrisha Maovu na kukataza mema' Tukiachana na nafsi zetu – hili tutakuja kulizungumzia siku nyingine namna gani ya kujiepusha na vishawishi vya nafsi. Leo nitajitahidi kuzungumza nawe njia sita nyepesi ambazo kwa uwezo wa Allaah tunaweza kufanikiwa kujiepusha na Sheitwani na kuweza kuepuka maasi ambayo tumekatazwa.
Tambua kuwa Sheitwani yupo
Katika
njia rahisi ya kuweza kupambana na adui yeyote kwanza ni lazima ujue kwa dhati
kwamba yupo, na ikiwezekana ujue namna ya utendaji kazi wake na ujue udhaifu
wake. Hivyo jambo muhimu kabisa ni kujua kuwa huyu shetani yupo, na ni lazima
ujue kuwa yupo shetani wa ki jini ambaye haonekani lakini pia yupo shetani wa
kibinaadamu ambaye ananonekana na anaweza kuwa mtu yeyote katika walio
kuzunguuka. Baada ya kujua sasa fanya mbinu hizi kumuepuka na kutokukuingiza
katika masuala ya madhambi.
1. Yajue ya haramu
Nafikiri iko wazi kuwa kila
mtu anayajua mambo ambayo ni haramu ambayo Allaah amekataza tusifanye. Hivyo
unatakiwa kuyatambua kutoka ndani ya nafsi yako na kujua kuwa kuyafanya haya ni
makosa makubwa. Hii ifanye iwe ni sehemu yako ya maisha ya kila siku. Kabla
hujafanya jambo / kuzungumza chochote ni lazima upime katika mizani ya dini
kuwa ni haki kufanya au LAA.
2. Zijue adhabu za AllaahYJH7
Soma, sikiliza, uliza na
ufahamu juu ya adhabu atakazo adhibiwa
mtu mwenye kufanya maovu. Jua kuwa Mungu yupo na adhabu zake ni kazi na zipo
kwa ajili ya yeyote ambaye atakiuka mipaka yake.
3. Tambua madhara ya kila ovu. Duniani na akhera
Tambua madhara ya kila ovu
ambalo unakusudia kulifanya. Kila ambalo limekatazwa ujue lina madhara kuanzia
hapa duniani na kesho Akhera.
Mfano ni jambo la ZINAA
jambo hili madhara yake yako wazi kabisa kuanzia EDChapa duniani na kesho akhera.
Tulijaribu kueleza madhara ya zinaa kwa uchache kwa hapa duniani. Kama mada hii
uliikosa unaweza kupitia hapo chini kabla ya kuendelea.
4. Tambua umuhimu wa Kumcha Mungu
Mche Mungu, mtaje Mungu
kila wakati, tambua kuwa Mungu anakuona kila nukta ya maisha yako. Wengi wetu
tunasali na kufunga tu kwa kufuata mkumbo hatujawa na imani thabiti kwRTFGVBa Allaah.
Hivyo tunapaswa kumjua Mwenyezimungu kwa kina kabisa ili tukijue kile
tunachokifanya.
5. Isome na uisikilize sana Quran
Si wote tunaweza kuielewa
Quran na maana yake, lakini sote tunatakiwa kuisoma, kuisikiliza na kufuata
yaliyomo Najua uko bize sana na dunia yetu ya leo lakini jaribu
kutenga muda walau wa dakika 30 ndani ya siku nzima ujaribu kupitia maneno haya
matukufu ambayo ndio muongozo wa Muislamu (QURAN). Na kama sehemu yako ya kazi pana
utulivu jitahidi sana badala ya kusikiliza muziki basi usikilize Quran/mawaidha. Siku
hizi pia ulimwengu umekuwa rahisi kusoma Quran sio mpaka uwe na Msahafu, Quran unaweza kuipata kwenye simu na kwa lugha yako wewe ambayo unaelewa na unaweza
kusoma maana na tafsiri yake kwa urahisi kabisa.
6. Msimamo binafsi
Baada ya kuyajua hayo kuwa
na msimamo wewe kama wewe, usiwe mwepesi kushawishiwa na kitu kingine kama
nafsi na mtu mwingine. Ingawa nafsi nayo hua inaamrisha maovu muda mwingine,
unatakiwa kuidhibiti kwani hata sheitwani wa kijini anapotaka kukushawishi
hupitia katika nafsi yako.
HITIMISHO
ALLAAH anasema katika Quran
“Hakika Sheitwani kwenu nyinyi ni adui
nasi tunatakiwa tumfanye kuwa ni adui”
Na kwa kumalizia tu naweza
kusema kuwa yote hayo yanahitaji subira ya hali ya juu sana. Kwani katika hali
ya kawaida mambo ya maasi yamepambwa sana na yanavutia katika macho ya mwenye
kutazama ma katika masikio ya mwenye kusikiliza. Mfano mdogo tu ni vishawishi
ambavyo tunaviona katika sehemu mbali mbali za maisha yetu, makazini,
barabarani, majumbani n.k. Lakini pia maasi yamepambwa sana katika masikio ya
mwenye kusikiliza mfano ni nyimbo na mambo mengine ya upuuzi. Kiukweli kabisa
hakuna atakaye toka katika mabano haya ila ni kumtegemea sana Mwenyezimungu na
kuazimia hasa katika hilo.
KWANINI?
Kwa sababu tumekuwa ni Umma
bora, kwakuwa tunaamrishana mema na kukatazana maasi. Hivyo jukumu hili sio la
mashekhe peke yao bali ni la kila mmoja. Kwa kuwa nami ni mmoja katika
Umma huu bora nimeona niitumie fursa hii kuwaeleza jambo hili. Kama
utapata wasaa nawe ni bora ukashea na
mwingine walau kwa uchache aipate elimu hii.
Makala hii fupi imeandaliwa
na kuandikwa na Saidi Bunduki kutoka katika mtandao wa mrbunduki.com
Baadhi ya Darasa muhimu zilizopita
Salaat Al istikhaara
Adabu za kusoma Qur ani
Maana ya swala
MWENYEEZIMUNGU NDIYE MJUZI ZAIDI
Baadhi ya Darasa muhimu zilizopita
Salaat Al istikhaara
Adabu za kusoma Qur ani
Maana ya swala


COMMENTS