
MIJI YA KALE ZAIDI DUNIANI AMBAYO BADO IPO HADI LEO
Nadhani utakubaliana nami kuwa hakuna anayejua uhakika wa umri wa dunia tangu kuwepo kwake ila ni Mwenyezimungu tu.
Pamoja na hayo, Mwanadamu aliishi miaka mingi mbayo nayo pia hakuna anayejua umri halisi tangu enzi hizo.
Lakini katika kumbukumbu ambazo zimebahatika kuhifadhiwa zipo sehemu ambazo ni za zamani zaidi.
Leo nimekusogezea dondoo za miji ya kale zaidi ambayo ipo mpaka leo
FUATANA NAMI
Muandaaji wa makala hii ni mimi;-
Maoni yako, ushauri na rai yako ni muhimu kwetu, hivyo baada ya kusoma makala hii ni vema ukatuandikia maoni yako hapo chini katika sehemu ya COMMENTS.
1. JERUSALEM

2. VARANASI
Licha ya kuwa ni miongoni mwa miji mikongwe zaidi INDIA lakini kwa wahindu huu ni mji mtakatifu zaidi kuliko yote ulimwenguni na ni sehemu ambayo hufanya hija.

3. LUOYANG

4. RAYY
Mji huu unapatikana katika Nchi ya IRAN karibu na mji mkuu "Tehran"
Mji huu unasadikika kuwepo miaka zaidi ya elfu 6 tangu kuanzishwa kwake.
6. SIDON
Mji ambao ulikaliwa kwa zaidi ya miaka elfu 6 wa Sidon na pia ulikuwa ni mji muhimu kwa sababu ya kuwa na bandari kuu katika bahari ya Mediterranea. Mji huu unapatikana katika nchi ya LEBANON.
6. ALEPPO
Utafiti unaonesha mji huu kuwepo zaidi ya miaka elfu 13 huko nyuma. Ni miongoni mwa makazi ya zamani zaidi ya binadamu hapa duniani. Mji huu unapatikana katika nchi ya SYRIA.
Aleppo ni miongoni mwa miji yenye idadi kubwa ya watu, ingawa vita vya wenyewe kwa wenyewe viliathiri sana idadi na shughuli za kiuchumi kwa ujumla.
7. FAIYUM
Moja katika nchi za Afrika ambazo zina historia nyingi za kujifunza mambo mbali mbali ni nchi ya MISRI (Egypt).
Moja kwa moja hapa tunakutana na mji huu wa Faiyum pembezoni mwa mto Nail. Mji huu unasadikika kuwepo miaka elfu 4 iliyopita. Kulingana na hali ya ukame watu wengi walihama mji huu na kupelekea mpaka sasa mji huu.
8. PLOVDIV
Mpaka kufikia leo, mji huu ni mji wa pili kwa ukubwa katika nchi ya BULGARIA. Hapo awali mji huu ulitawaliwa na wasunni, wagiriki na hatimaye warumi. Lakini pia ulitawaliwa na watomania kwa muda.
Mji huu ulikuwepo miaka 6000 iliyopita nchini humo.
9. ARGOS
Huu ni moja katika miji ambayo ilikuweko miaka mingi iliyopita katika bara la Ulaya. Mji huu unapatikana katika nchi ya GREECE (UGIRIKI)
10. DAMASCUS
Damaskas ni mji miongoni mwa miji mikongwe ulimwenguni, ulikwepo zaidi ya miaka elfu 11 iliyopita. Mji huu unapatikana katika nchi ya SYRIA. kwa sasa mji huu una wakazi zaidi ya milioni 2.5
Leo tunakomea hapa, Je? kuna mji wowote ambao hatujautaja? Tuandikie hapo chini katika sehemu ya COMMENTS
Usisahau kushea na mwenzio kupitia mitandao ya kijamii hapo chini.
Ahsante
*********************
Duh...tumetoka mbali
ReplyDeleteSana
ReplyDelete