je WAJUA?
Inakadiriwa kuwa Ndani ya bahari kuna samaki zaidi ya 3,500,000,000,000 (yaani 3.5 trilioni) wakiwa wamegawanyika katika aina zaidi ya elfu 28 (28,000)
Lakini hiyo sio ishu sana, ishu nikwamba kuna wale ambao wametengeneza jina kutonakana na ukubwa wao na umaarufu wao. Leo nakuwekea hapa aina 8 ya samaki wakubwa zaidi duniani wanaoishi mpaka leo katika bahari mbali mbali za hapa ulimwenguni.
8. THE GREENLAND SHARK
Huyu ni samaki aina ya papa ambaye anavunja rekodi kwa jinsi alivyo. Kwanza anaishi katika mazingira ya bahari yaenye baridi kali sana katika nyuzi joto sentigredi 2 mpaka 7. Pia Ana uwezo wa kuishi umri mpaka miaka 400. Urefu wake unaweza kufikia mpaka mita 7.2
7. GIANT PACIFIC OCTOPUS
Huyu ni pweza ambaye anaishi bahari ya pasifiki. Anakadiriwa kuwa na urefu wa mita 9 na uzito wa kilo mpaka 180.
6. REGALEC
Inasemekana kuwa huyu ndiye samaki mrefu zaidi katika samaki wenye mfupa hapa duniani. Kutokana na uchunguzi wa hivi karibuni samaki huyu inasemekana kuwa anaweza kufikia urefu wa mita 11 na uzito wa kilo 270.
5. BASKING SHARK
Huyu ni papa wa pili kwa ukubwa katika papa ambao huishi katika maji yenye joto. Hupatikana katika bahari ya Atlantic na bahari ya Pasifiki.
4. GIANT SQUID
Samaki hawa wanatofautiana ukubwa baina ya wanawake na wanaume ambapo samaki wa kiume anakadiriwa kufikia mpaka urefu wa mita 10 wakati wakike hufikia mpaka mita 13. Samaki hawa hupatikana chini zaidi ya bahari katika kina cha mita 500 na kuendelea ambapo baadhi ya nyangumi nao huishi huko.
3. COLOSSAL SQUID
Huyu ndo samaki mwenye macho makubwa zaidi ambayo yanakadiriwa kufikia sentimeta 27 (27 cm). Uchunguzi zaidi unaendelea juu ya samaki huyu.
2. WHALE SHARK
Huyu ni samaki aina ya nyangumi, huyu ndiye samaki mkubwa zaidi duniani. Inasemekana kuwa anaweza kufika urefu wa mita 20.
1. CYANEA CAPILLATA
Huyu ni samaki aina ya Jellyfish mkubwa zaidi duniani ambaye anaweza kufikia urefu wa hadi mita 40.
Asante kwa kuwa nasi.
Makala hii fupi imeandaliwa na mtandao bora kabisa wa mrbunduki.com

Shukran sana
ReplyDelete