Wanaita mimba mikubwa. Yaani mtu mwingine mpaka kutembea inakuwa shida. Sababu ni hizi hapa
Mara nyingi unaweza kujiuliza ni kwanini kuna baadhi ya wanawake akiwa na ujauzito tumbo linakuwa kuuubwa kupita kiasi?
Unaweza kuhisi labda amebeba mapacha ama mtoto ni mkubwa kupita kiasi. Lakini jibu laweza kuwa NDIO au HAPANA. Lakini je inapokuwa ni kinyume na hivyo nini hasa sababu zinazopelekea hivyo?
ZIPO SABABU KADHAA ZA KITAALAMU NIMEKUWEKEA HAPA CHINI
Hebu tuone sababu hizi 5.
imeandaliwa na www.mrbunduki.com
Usisahau kutupia Comment yako sehemu ya chini kabisa baada ya posti hii.
1. KIMO CHA MAMA MJAMZITO
Sababu hii huchukua nafasi kubwa katika hili. Mama anapokuwa mrefu zaidi ni rahisi tumbo kuwa kubwa na refu lakini akiwa mfupi zaidi sehemu ya tumbo huwa ndogo na kusabisha tumbo kukua kuelekea mbele.
2. UKAAJI WA MTOTO TUMBONI
Fahamu kuwa mtoto huwa anakuwa na mikao tofauti tofauti. Hivyo hii inaweza kuwa ni sababu ya tumbo kuwa kubwa.
3.MAJI YA AMNIOTIC (AMNIOTIC FLUID)
Hii inaweza kuathiri ukubwa wa mtoto mapema zaidi. Wataalamu wa mambo ya afya ya uzazi wanasema kuwa kipimo cha maji haya inatakiwa isizidi lita moja. Inapozidi zaidi ya hapo ndipo tumbo linaweza kuwa kubwa zaidi na hatimaye kuhitaji matibabu mbadala.
4.UKUBWA WA MTOTO
Ukiachana na sababu hizo hapo juu lakini pia ukubwa wa mtoto ni moja ya sababu zinazosababisha tumbo la mimba kuwa kubwa zaidi. Lakini pia baadhi ya magonjwa kwa mama mjamzito huweza kusababisha tatizo hili ikiwemo kisukari.
5. MAPACHA
Tumalize na sababu hii maarufu.
Kwa walio wengi akiwa na tummbo la watoto zaidi ya mmoja ni lazima kuwa kubwa ingawa sio wote.
Kwa walio wengi akiwa na tummbo la watoto zaidi ya mmoja ni lazima kuwa kubwa ingawa sio wote.
Asante kwa kuwa nasi
Safi,
ReplyDeleteNice boss
ReplyDelete