Ukiachana na maajabu 7 ya dunia, haya ni maeneo ambayo yamegunduliwa na yatakushangaza
Dunia na maajabu yake
Huenda umeshasikia mengi katika maajabu ya dunia, lakini usisikie haya. Leo nakudokeza baadhi ya sehemu tano ambazo zimeshangaza wengi katika ulimwengu huu.
'Nakukumbusha tu usisahau kuweka comment yako hapo chini kwa maoni, ushauri, mapendekezo n.k.
1. GATES OF HELL
Eneo hili linapatikana
katika nchi ya URUSI (Rusia). Eneo hili ni kama shimo kubwa linalowaka moto
ambao hauzimi.
Inasemekana kuwa eneo hili liligundulika hapo zamani na inasemekana kuwa kulikuwa na GAS, lakini katika harakati za uchimbaji wa gas hiyo ndipo
ukazuka moto huo na mpaka leo bado haujazima. Jina hili maana yake ni ‘Lango la
kuzimu’
2. PINK LAKE HILLIER
Eneo hili hupatikana nchini Australia, haya ni maji ya ziwa lenye rangi ya pink. Hii ni tofauti na tulivozoea kuyaona maji ya ziwa. Kwa kawaida maji ya ziwa huwa na rangi ya buluu japokuwa maji hayana rangi. Sasa katika ziwa hili rangi yake ni tofauti kwani hatujawahi kuona maji yakiakisi rangi ya pink.
3. VOLCANIC LIGHTNING
Kawaida ya volcano huwa ni hatari kulingana na mlipuko wake, lakini volcano hii ni hatari zaidi kutokana na mfumo wake. volcano hii hutokana na radi pamoja na umeme.
4. REFLECTIVE SALT FLATS
Eneo hili ni mfano wa kioo, ukijitazama chini unajiona, na ni eneo kubwa la kutosha. Lipo katika nchi ya Bolivia upande wa kusini magharibi karibu na eneo la Andes. Eneo hili lina takriban urefu wa zaidi ya kilomita 130
5. SHIMMERING SHORES OF VAADHOO MALDIVES
Hapa ni beach yenye maji yakawaida tu, ila ajabu yake ni kwamba ukiyapiga ama yakipigwa na upepo yanakuwa na rangi kama ya shoti ya umeme. Hali kadhalika mawimbi yake nayo yanakuwa vivyo hivyo. Kisiwa cha Vaadhoo ni miongoni mwa visiwa vya Maldives.

Nafikiri utakuwa umejifunza kitu katika makala hii, basi ni vema ukashea na mwingine naye aweze kujifunza na kujua machache katika mengi yaliyoko katika dunia yetu.
Gates of hell ilianza kuwaka toka 1971 mpaka hivi leo. Moto huu uliwashwa kwa makusudi na wataalamu wa Jiolojia (geology).
ReplyDeleteEneo hili lenye kina cha mita 30, lilikuwa likitoa gesi ya methane. Gesi hii ni hatari kwa maisha ya viumbe endapo ingeendelea kusambaa duniani.
Ili kuizuia gesi hii isisambae wanasayansi wakaona njia pekee ni kuiwasha moto. Hivyo kila ikitoka inakutana na moto na inawaka. Nizaidi ya nusu karne sasa sasa moto unawaka na gesi inazidi kutoka.
Duuh simchezo aisee
ReplyDeleteAsante mkuu
ReplyDeleteShukran
Delete