Ukiachana na mbu ambao hueneza malaria, lakini pia wapo mbu ambao hueneza ugonjwa uitwao dengue
Ugonjwa huu husababishwa na virusi DENGUE na ni miongoni mwa homa zinazosababishwa na kuenezwa na MBU aina ya AEDES. Na ugonjwa huu una uhusiano mkubwa na ugonjwa wa homa ya manjano
Dalili zake huweza kujitokeza kuanzia siku ya tatu mpaka kumi na nne tangu kupata maambukizi.
DALILI ZAKE
Miongoni mwa DALILI kubwa za ugonjwa huu ni pamoja na
1. homa kali
2. Maumivu ya kichwa
3. Kutapika
4. Maumivu ya misuli
5. Vipele katika ngozi
MATIBABU
Hakuna dawa maalum ya ugonjwa huu, ila kama utapata maambukizi basi unashauriwa kufanya yafuatayo;-
- Kupumzika
- Kunywa maji mengi
KINGA
- Njia iliyo bora zaidi ya kujikinga na ugonjwa huu ni kuzuia kuumwa na mbu kwa kutumia chandarua chenye dawa ama dawa nyingine za mbu hasa kama unaishi ama kusafiri maeneo ya kitropiki.
Punguza / ondoa kabisa masalia na maeneo yote ambayo mbu huzaliana
- Uonapo dalili za dengu basi mapema muone daktari.
COMMENTS