![]() |
Bila shaka kuna siku umeshawahi kuingia katika mtandao wa google na kukuta mabadiliko katika ukurasa wake wa nyumbani? "Home page" Mabadiliko hayo yaweza kuwa ni katuni, picha, music n.k
Sasa hizo ndizo google doodles ambazo nitakudokeza leo.
Itapendeza zaidi baada ya kusoma makala hii, shuka chini sehemu ya Comment na utuachie maoni yako, ushauri n.k.
Google doodles ni nini?
Hizi ni zana zinazokuwepo katika ukurasa wa nyumbani wa google (HOME PAGE) kama unavoonekana hapo katika picha.
![]() |
| Google 'HOME PAGE' |
Mara nyingi sanaa hizi za picha hutumika kuonyesha matukio ya kumbukumbu za kihistoria, mambo ya kupita katika historia ya dunia na mambo mengine ya kiulimwengu kwa lengo la kutoa taarifa kwa umma.
Mara nyingi huwa katika sura ya katuni (vibonzo), maandishi n.k.
Kwakuwa google ni mtandao mkubwa sana ulimwenguni na watu wengi huutumia, hivyo sehemu hii (Home page) huwa kama ubao wa matangazo/taarifa kwa umma (kwa watumiaji wake).
Google doodles Ilianza lini na nani alianzisha?
Utaratibu huu ulianza zamani tangu mwaka 1998 ingawa ulikuwa haujawa rasmi kama ilivyo leo.
George Larry na Sergey Brin hawa ndio waanzilishi wa mtandao wa google na ndio walikuja na wazo hili walipohudhuria tamasha la Burning man huko Nevada nchini Marekani.
Doodle ya kwanza ilikuwa ikifanana na nembo ya Burning man.
Kukua kwa google doodles hadi kufikia leo kuwa maarufu
Miaka takriban miwili tangu kuanzishwa kwake, mnamo mwaka 2000 bwana mmoja aitwaye Denis Hwang aliombwa kuunda doodle ya Bastille day na doodle hiyo ilifanya vizuri sana mtandaoni na hatimaye viongozi wa Google kuamua kumuajiri ili kusimamia kitengo hiki na kuwa rasmi.
Kwasasa google imeajiri wachoraji na wabunifu wenye vipaji kwa ajili ya kuweka michoro ambayo huelezea juu ya jambo fulani mfano wakati wa janga la corona n.k.
Mara kadhaa pia google doodles hujumuisha michezo ya kufurahisha pale ambapo utakuwa umebonyeza picha ile kabla ya kuona lengo husika ama ujumbe uliowekwa.
Hizi ni baadhi ya Doodles maarufu zaidi kwa mwaka 2020;-
Jaruary 19 – Ilisherehekea siku ya Martin luther King JR.
February 29 – Ilisherehekea siku ya Leap (Leap day)
March 19 – Mwanzo wa msimu wa masika
April 2 – Ilitoa vidokezo kuhusu Coronavirus “Baki nyumbani okoa maisha”
Nawezaje kuona Doodles zilizo pita?
Endapo umepitwa na moja kati ya doodles za google na unataka kuziona basi unaweza kuzipata kwa utaratibu ufuatao
Ingia katika mtandao wa google kisha andika ‘google.com/doodles’ hapa utapata kumbukukumbu zote.
Asante kwa kuwa nasi katika makala hii fupi ya teknolojia.
Lakini pia unaweza kupitia makala zetu mbali mbali za mada tofauti zikiwemo AFYA, PICHA NA MATUKIO, MIKASA n.k.


Shukran
ReplyDelete