Nani anaweza akatunza siri zangu ili niongee naye?
Nitaongea
Na Nani? Nimpe Yanonisibu
Siri Zangu
Za Moyoni, Awe Ana Ziratibu
Kwa Ukweli
Simuoni, Wote Wana Majaribu
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Na Mimi
Ni Mwanadamu, Yako Yanayoniuma
Huwa Nakuwa
Na Hamu, Vikwazo Vyangu Kusema
Nimwambie
Nani Humu, Atae Nitunza Jama
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Ni Mengi
Yananikwaza, Moyo Umejaa Kutu
Nalia Na
Kunyamaza, Moyo Wa Mtu Msitu
Sauti Nataka
Paza, Ila Naogopa Watu
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Mambo Mengi
Yaniliza, Zaidi Ya Hamsini
Mchana Kwangu
Ni Kiza, Sina Raha Maishani
Mengi Yananiumiza,
Mwaminifu Simuoni
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Nimuamini
Fulani?, Ila Yule Domo Kaya
Zitafika
Mtaani, Na Siri Zangu Ni Mbaya
Nimwambie
Wa Pembeni?, Huyu Naye Hana Haya
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Nimwambie
Huyu Bwana?, Huyu Ana Kisirani
Siku Tukiparangana,
Atamwaga Vyote Chini
Huyu Sio
Muungwana, Tanitia Hatiani
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Nimwambie
Yule Pale? Yule Kajawa Dharau
Simmwagie
Mchele, Leo Kesho Kasahau
Mwanzo Wa
Ngoma Ni Lele, Mwisho Apindua Dau
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Nimpe Nani
Za Moyo? Siri Zangu Awe Nazo
Kila Nimwonae
Siyo, Kubeba Hana Uwezo
Nabaki Piga
Miayo, Najiongeza Mawazo
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Moyo Wangu
Waniuma, Umejawa Taharuki
Mengi Yananisakama,
Tena Ni Mengi Lukuki
Naenda Mikono
Nyuma,Kichwa Chini Hakitoki
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Kila Mtu Anawaza, Ila
Mengine Puuo
Mawazo Yanaumiza,
Usikie Kwa Wenzio
Mwenzenu
Yananiliza, Najikaza Ki Chanuo
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Moyo Wangu
Ni Mgumu, Zaidi Ya Mwamba
Geu
Mambo Yaliyomo
Humu, Nyingi Ni Sitosahau
Nataka Punguza
Sumu, Nitulie Angalau
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Ya Rabbi
Nafsi Yangu, Naijutia Kwakweli
Yale Ya
Tangu Na Tangu, Ni Mengi Na Nishafeli
Muumba Watu
Na Mbingu, Nipoze Ewe Jalali
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Mungu Baba
Nisitiri, Walimwengu Hawawezi
Nitunzie
Zangu Siri, Nakuomba E Mwenyezi
Unitie Ujasiri,
Niuache Na Ushenzi
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
Nalia Chozi
La Maji, La Damu Limesha Goma
Kwa
Mannani Nataraji, Kupata Kilichochema
Ni Bahati
Si Kipaji, Kwa Haya Niliyosema
Nizungumze
Na Nani, Awezaye Tunza Siri?
SAIDI BUNDUKI @ 2018

COMMENTS