ILIPOISHIA...............
Hofu ilitanda sana hasa pale ambapo tumebanwa na kufukiwa na nyasi za kibanda, na hakuna ambaye aliwahi kutoka nje, kibaya zaidi mwenzetu anapiga kelele anaumia. Aisee niliogopa sana.
**************
ENDELEA
Mimi nilikuwa nimelala karibu na nje, hivyo nilijipenyeza chini ya uvungu wa kitanda chetu cha kichanja na kufanikiwa kutoka.
Kumbuka kuwa wakati huo mvua ilikuwa inanyesha sana. Baadaye na mwenzangu mwingine alitoka na tukaanza kuwasaidia wenzetu ambao walikuwa wamebanwa na miti pamoja na nyasi za kibanda.
Nakumbuka jamaa mmoja alikuwa amelala, kamwe hakujua kinachoendelea. Huyu jamaa bwana alikuwa na usingizi sana huenda alikuwa na ule ugonwja wa kupenda kulala sana
- Kama unataka kuufahamu UGONJWA huo soma Makala hii hapa chini
Ufahamu ugonjwa wa kupenda kulala sana (CLINOMANIA)
Mtihani ulikuwa ni wapi tutaeleka baada ya kibanda chetu kuanguka, ukizingatia ule ni usiku wa saa saba.
Kwa mbali kulikuwa na jirani yetu ambaye tulizoeana naye, Kiongozi wetu aliamuru kuwa tujaribu kuelekea kwa jirani yetu kuomba hifadhi ya kulala.
Mungu alibariki tulipata hifadhi na siku ile ikapita vema.
Siku ya pili tulilazimika kusitisha kazi na kuendelea na shughuli za kujenga kibanda kilicho madhubuti zaidi ya kile baada ya hapo tuliamua kuendelea na kazi zetu kama kawaida.
Siku moja tukiwa tumelala majira ya saa kumi na moja alfajiri tulifikiwa na taarifa ya kusikitisha sana, hii ni taarifa ya ajali ambayo ilitokea Tanga mjini na baadhi ya wanafunzi wenzetu zaidi ya 17 kufariki kwa ajali ile wakitokea Maulidini.
Kama uliikosa stori hiyo soma hapa
Baada ya muda mrefu wa kumaliza msiba wa ndugu zetu wanafunzi tulirudi tena shamba kumaliza kazi yetu tukiwa na majonzi sana lakini Mungu ndio alipanga vile.
Ukiachana na waliofariki pia wapo ambao walipoteza viungo vyao mbali mbali kama mikono, miguu na wengine kupata majeraha makubwa na madogo na wachache kunusurika kabisa.
Siku moja tukiwa shambani katika ile awamu ya pili, ilikuwa ni majira ya saa sita mchana tukimalizia ngwe yetu ya asubuhi, nilishtuka ghafla kichwa kikiwa kinaniuma sana. Kichwa kiliuma sana kiasi kwamba nilijikaza kakini sikuweza kuendelea na kazi.
Kiongozi wangu aliniambia niende nikapumzike kibandani nami nikafanya hivyo. Kichwa kiliniuma sana na baridi kali mno, nililala na kujifunika shuka lakini bado nilihisi baridi ya ajabu.
Baadaye walipika chakula lakini nilishindwa kula kutokana na hali yangu ya ugonjwa.
Hofu ilitanda dhidi yangu kiasi kwamba wenzangu waliniamuru kuwa niende nyumbani kwani safari hii kwa bahati mbaya tulisahau hata dawa za akiba.
Nitakwendaje nyumbani wakati nilikuwanaumwa sana? Na mahala ambapo tulikuwa ni mbali sana na barabara ili kupata gari, sehemu ambayo nilitakiwa kutembea kwa mguu, na muda tayari ilikuwa ni saa 11 jioni.
ENDELEA...
Nililazimika kutoka pale mdogo mdogo kuelekea barabarani ambako ningepata usafiri. Umbali wa pale shambani hadi ilipo barabara ni zaidi ya kilomita 15. Hapa sitosahau kwakweli
Niliianza safari Nikiwa na nguo zangu ambazo nilikuwa nikifanya nazo kazi kule shambani huku mkononi nikiwa na kimfuko changu cha rambo ambacho niliweka nguo nzuri ili nikazivae mbeleni.
Nilipita katika mto mmoja hivi na kuwakuta watoto wengi wakike wakichota maji.
Mabinti wale waliponiona kutokana na muonekano wangu kuwa kama kichaa maana nilichafuka sana, basi mabinti wale walianza kunizomea na kunicheka. Dah kutokana na hali yangu jinsi ninavoumwa hata kutembea ilikuwa ni shida, kiukweli sikuwajali na niliendelea na safari yangu.
Nilitembea sana hatimaye jua likazama kiza kikaingia, baridi ilinizidi sana mwilini mwangu kiasi cha kunifanya nipunguze mwendo na hatimaye nishindwe kabisa kutembea.
Niliamua kukaa chini ya shamba moja kando ya barabara na kupumzika nikisubiri kama hali itakuwa nzuri kiasi ili niendelee na safari.
Hali iligoma kutengemaa na mara likafunga wingu kubwa la mvua, niliamua kuamka na kujikongoja kuendelea na safari yangu ngumu. Wingu lile lilikuwa zito kiasi kwamba mda wowote lingenyesha
Niliwaza sana na kuogopa hasa ukizingatia na baridi ambayo nahisi, laiti mvua ile ikininyeshea nitakuwa katika hali gani mimi?
Niliamua kumuelekea Mungu na kumuomba kwa dhati kabisa kuwa aniepushe na mvua ile mpaka nitakapofika sehemu ambayo nitapata hifadhi. Kabla sijamaliza maombi mvua ikaanza kudondoka kwambali…
Daaaah……….. SITOSAHAU
ITAENDELEA.................

COMMENTS