Kama sio wewe basi ni rafiki yako. Hua anapenda saaana kulala kila wakati. Basi anasumbuliwa na ugonjwa huu wa CLINOMANIA
👇_______________👇
Kawaida ya mwanadamu ama watu wengi huwa wanapenda na wanafurahia kulala. Lakini upo ugonjwa wa kupenda kulala zaidi ambao kitaalamu hujulikana kama CLINOMANIA.
*************************
- Mtu mwenye ugonjwa huu, hupenda kulala bila kikomo na huchukia kuamka. Huyu hupenda kulala kuliko kawaida.
Hizi ni miongoni mwa dalili zake chache ambazo huashiria ugonjwa huo.
1. Kutokuchoka kulala.
Yaani mda wowote iwe mchana, asbuhi, usiku wewe unajiskia kulala tu.
2. Kupenda kuwa kitandani mda wote
Unapenda kufanya mambo yako yote ukiwa kitandani ili uwe katibu na usingizi. Vitu kama kula, kunywa, kusoma hupenda kuvifanya ukiwa kitandani
3. Kuijiskia furaha pale unapopata fursa ya kurudi kitandani
4. Starehe yako kubwa zaidi ya zote kuwa ni kulala
Tiba yake ni kupata msaada kwa wana saikolojia na wataalamu wa mambo hayo.
ANGALIZO
Pindi uonapo dalili hizo ni vema kuwaona wataalamu wa afya.
COMMENTS