Fahamu walau kwa uchache kuhusiana na ugonjwa wa ini
UGONJWA WA HOMA YA INI
Kama tunavofahamu kuwa Moja katika viungo muhimu vilivyo katika mwili wa binadamu ni INI.
Wataalamu wa mambo ya afya wanasema kuwa ini lina kazi zaidi ya 400 lakini kubwa katika hizo ni kuchuja na kuondoa sumu katika damu.
SABABU ZA UGONJWA WA INI
NI MAMBO YAPI HASA HUSABABISHA UGONJWA HUU?
- Unywaji wa pombe kupitiliza imekuwa ni chanzo kikubwa cha ugonjwa huu, lakini pia sumu katika damu husababisha kuvimba kwa ini na kusindwa kufanya kazi ipasavyo na husababisha ugonjwa huu ambao kwa kitaalamu huitwa HEPATITIS
AINA ZA VIRUSI VYA UGONJWA WA INI
Virusi vya ugonjwa wa Ini vimegawanyika katika aina 5 ambazo ni A, B, C D na E wakati B na C ndivyo huathiri kwa zaidi ya asilimia 95.
- Homa ya ini ni miongoni mwa magonjwa ambayo huuwa zaidi watu
VIPI UNAWEZA KUAMBUKIZWA UGONJWA WA INI?
Virusi vya homa ya INI husambaa kupitia maji maji ya mwili kama vile Damu, Manii, Mate na maji mengine mwilini. Hivyo basi tunaweza kuona kuwa ugonjwa huu husababishwa kupitia;-
- Kujamiiana na mtu mwenye maambukizi bila kutumia kinga
- Kutoka kwa mama mwenye maambukizi kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua
- Kuongezewa damu ya mtu mwenye maambukizi
- Kuchangia baadhi ya vitu na mtu mwenye maambukizi. mfano miswaki, taulo, vitu vyenye ncha kali kama wembe, sindano n.k
NI ZIPI DALILI ZA UGONJWA WA INI?
Mara nyingi ugonjwa huu huwa hauna dalili, mtu anaweza kukaa nao kwa muda mrefu bila kujijua huku akiwaambukiza wengine. Lakini baadhi ya dalili zake kwa baadhi ya watu ni pamoja na;-
- Kupoteza hamu ya kula
- Mwili kuchoka
- Kichefuchefu na kutapika
- Mabadiliko ya mkojo na kuwa rangi nyeusi mfano wa COCACOLA
Dalili nyingine ni;-
- Kupungua uzito
- Macho na ngozi kuwa na rangi ya njano kama unavoona hapo katika picha ya chini
![]() |
| Jicho na ngozi ya muathirika |
NI IPI TIBA YA UGONJWA WA INI
Mpaka sasa ugonjwa huu hauna tiba maalum kwani ini likishafika kiwango cha kuharibika au kupata saratani ya ini basi kifuatacho hapo ni kifo.
Lakini badala yake ipo tiba ya lishe ambayo hufaa kutumia kutokana na tatizo hili kuwa kubwa na kuathiri wa tu wengi.
Hizi ni Natural antibiotics ambazo husaidia kuuwa bakteria na vizus pamoja na kuzipa nguvu kinga za mwili. Lakini pia
- Huupa nguvu mwili
- Kuongeza virutubisho na kujenga afya bora
- Kuondoa magonjwa nyemelezi
Pamoja na ugonjwa huu kuwa hatari kwa watu wote, lakini yako makundi ya watu ambayo yapo katika hatari zaidi kupata maradhi haya.-
- Watoto wachanga (walio zaliwa na maambukizi kutoka kwa mama)
- Wanaofanya biashara za ngono (kujiuza)
- Wanaume wafanyazo mapenzi ya jinsia moja
- Wanaojidunga dawa za kulevya
- Mwenye mpenzi mwenye ugonjwa huu
- Wanaoishi na mgonjwa wa ini
- Wafanyakazi wa huduma za afya
'CHANJO YA UGONJWA WA INI'
Chanjo ya ugonjwa wa ini ni sindano tatu. Yakwanza ni baada ya kupimwa, ya pili ni baada ya mwezi mmoja na ya tatu ni baada ya miezi sita.
Ni muhimu zaidi kuwapatia chanjo watu hawa-
- Watumiaji wa madawa ya kulevya
- Watoto wote
- Ambao wamefanya mapenzi na mtu zaidi ya mmoja ndani ya kipindi cha miezi 6
- Wenye maradhi ya kudumu ya ini
- Wafanya biashara ya ngono
- Wanaoishi na waathirika
- Lakini pia chanjo ni muhimu kwa watu wote. Kwani hatujui ni nani kati yetu ameathirika
TANBIHI / UZINDUSHI
Virusi vya ugonjwa wa ini vina uwezo wa kukaa nje ya mwili kwa zaidi ya siku saba vikiwa bado na uwezo wa kumuambukiza mtu mwingine. Hata vikiwa vimekauka mfano kama ni damu au maji maji katika nguo.


COMMENTS