Basi bwana;-
Jamaa alikuwa ameshika kisu mkononi akaanza kutulisha machungwa, yeye anamenya na sisi tunakula zamu kwa zamu. Akimenya la kwanza nakula mimi, akimenya la pili anakula mwenzangu.
Utaratibu ukawa huo, na jamaa huwezi kuamini bwana hacheki na mtu.
- Kama umepitwa na sehemu ya kwanza ya kisa hiki basi bonyeza HAPA
Nilikula machungwa kama matatu au manne hivi, nikaona nyokoooo hapa nitakufa bure, ngoja nibuni uongno wowote ili niweze kuepukana na kadhia hii. Kiukweli kilichoniponza mimi ni tamaa tu ya kumfuata yule dogo katika sakata lake la kuvamia shamba la watu.
Nikamwambia yule jamaa braza e sikiliza, unajua mimi ni mgeni hapa na mwenyeji wangu ni huyu bwana, na yeye ndiye ambaye amenishawishi tule haya machungwa sasa mimi sina kosa blaza.
Bradha akasema usinitanie, hapa mtakula machungwa mpaka yaishe yote haya. Nyie si mnajifanya wezi wa machungwa ee. Inamaana we hujui kama hili shamba sio lenu? pumbav kabisa
Niliendelea kumsisitiza braza kuwa mimi sio mwizi na mwenzangu ndiye mwizi. Lakini hatimaye alikubali na kuniachia. Aisee nilikimbia kama gari ya mashindano nikimuacha mwenzangu akiendelea kupiga orange moja baada ya nyingine.😆
Nilipofika shamba kwa mjomba nikaulizwa bwana we hujakutana ya Yahaya huko?? Maana tumemtuma na ni muda mrefu sasa tunasubiri unga.
Itaendelea.............
***********
Je una kisa unataka kutuhadithia kupitia blog yetu?
Wote mnakaribishwa


COMMENTS