Mara nyingi hua napenda kuandika matukio ya safari zangu katika maisha. Pitia hii

Nimeipanga katika mtiririko huu;-
Furaha ilikuwa imeshamiri kwa kukutana na ndugu na jamaa zangu ambao kwa muda mrefi hatukua pamoja.
- KUONDOKA
- SHEREHE YA MAULIDI
- KURUDI MBEYA
- CHANGAMOTO ZA SAFARI
1. KUONDOKA
Niliondoka siku ya jumatano tarehe 12 / 08 / 2020 nikiwa katika basi la Kampuni ya SAULI LUXURY COACH.
- Safari ilianza mnamo saa 12:02 asubuhi
- Nilifika CHALINZE majira ya saa 11 jioni
Baada ya kufika chalinze nilipanda magari ya kuelekea Tanga kisha nikashuka katika kijiji cha Mkata ambapo nililala. Hapa nilifika majira ya saa 1:40 usiku.
Asubuhi nilikutana na mwanafunzi mwenzangu ambaye tulisoma wote Madrsatul maawa kule Mkalamo. Jamaa anaitwa Hakundwa Mohammed
Alinichukua na kwenda kupata chai nzito.
Niliondoka Mkata saa 4:46 asubuhi kwa basi la Kampuni ya KiDATO BUS SERVICE na Mwenyezimungu alinijaalia kufika Kijijini kwetu Mkalamo mnamo saa 8 mchana.
| My sweet Home |
Furaha ilikuwa imeshamiri kwa kukutana na ndugu na jamaa zangu ambao kwa muda mrefi hatukua pamoja.
Sikuweza kuwachukua wote katika picha, lakini hawa ni baadhi yao.
| Nikiwa na Kijana wangu - Salimu Mfano (Mwenye kanzu ya kijivu) |
| Hapa nikiwa na Ustadh AMIRI (wa katikati) na Ustadh ABDALA HAMISI |
| Hapa nikiwa na Ustadh ADAM BICHUKA (Mwenye Kofia) pamoja na BWN Mohamed Sindi |
2. SHEREHE YA MAULIDI
Sherehe ile ilipangwa kufanyika siku ya jumamosi tarehe 15 / 08 / 2020. Hivyo baada ya kufika ulikuwa ni muda muafaka wa maandalizi.
Miongoni mwa maandalizi makubwa ilikuwa ni kuandaa uwanja, kufunga taa, sambamba na kuweka maturubai.
| Ustadh Amiri akiwa na kijana wake Hamisi wakiwa katika maandalizi ya kufunga taa. |
Usiku wa kuamkia siku ya sherehe ilikuwa ni shamra shamra za hapa na pale nikiwa na baadhi ya vijana wa Madrasatul maawa ambao tulikesha kwa shughuli za utangulizi wa jambo letu.
Tarehe 15 ilipofika shughuli yetu ilianza majira ya saa 9 badala ya saa 8 ambayo tulipanga. Lakini hakuna ambacho kiliharibika.
Wanafunzi walikuja na kushiriki vizuri kabisa.
| Baadhi ya wanafunzi wa Madrasatul maawa, wakiwa wameshawasili eneo la tukio. |
Shughuli ilikwenda vizuri na kila mtu alifurahia kwa namna yake.
3. KURUDI
safari ya kurudi nilikuwa na familia yangu yote ambao wakati wa kwenda walitangulia kabla yangu.
Tuliondoka siku ya jumatano tarehe 19 / 08 / 2020 kwa basi la KIDATO majira ya saa 4:33 asubuhi.
Tulifika Mkata saa 8 mchana na baada ya kupata chakula tuliendelea na safari hadi kufika katika mji wa RUVU Mkoa wa PWANI ambako tulilala.
Hapa Ruvu ni kwa dada wa mke wangu.
Siku ya tarehe 20 tuliondoka Ruvu asubuhi saa mbili na kurejea Mbeya ambako tulifika saa 3:18 usiku.
4. CHANGAMOTO ZA SAFARI
Kwa kawaida kila jambo huwa halikosi changamoto zake. Miongoni mwa changamoto za safari yangu ni;-
i) USUMBUFU WA MIZIGO
Hii ilikuwa ni wakati wa kwenda, kwakuwa nilijiandaa kwenda kufanya shughuli ilinibidi kubeba mizigo mingi ikiwemo mchele, maharage na vinginevyo.
ii) UGUMU WA MAANDALIZI YA KIPINDI
Pamoja na maudhui mengine ya safari lakini pia nilikwenda kwa ajili ya kufanya kipindi cha "MAISHA SAFARI" na wadau mbali mbali ambao walipitia magumu katika maisha yao.
Kipindi hiki huwa kinaruka moja kwa moja katika channel yetu ya YOUTUBE ya Bunduki TV lakini pia hapa katika blog ya mrbunduki.com
Kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wangu, baadhi ya vitendea kazi vilikosekana na kusababisha kutokupata picha za video.
Lakini pia kutokana na mambo kuwa mengi, baadhi ya wadau sikuweza kufanya nao mahojiano na hatimaye kurudi Mbeya.
Hizi ni baadhi ya changamoto chache ambazo zilijitokeza katika safari hii.
Na huu ndio muhtasari wa safari yangu ya kuelekea Tanga.
**************
COMMENTS