Nufaika na silaha hizi TANO (5) madhubuti za uandishi ambazo zitamfanya msomaji kupeandezwa na makala zako kila siku.

Uhali gani mpenz msomaji wetu wa mtandao wako pendwa kabisa wa mrbunduki.com sambamba na Bunduki TV
Bila shaka ni mwenye afya tele, nasi tumefurahi kukuona hapa unaendelea kufuatilia makala zetu. Hatuna cha kukulipa ila Mungu yu pamoja nawe.
Leo nimeona nishiriki nawe elimu hii na si nyingine bali ni uandishi wa makala mbali mbali hasa katika blog na majukwaa mbali mbali ya mitandaoni na kwingineko.
Kwa jina jingine naweza kuiita mada hii kama
'MBINU ZA UANDISHI WA MAKALA'
Ulimwengu wa sasa watu wengi wamekuwa ni waandishi katika tasnia tofauti, kama vile habari za kila siku, makala mbali mbali na hata vitabu.
Baadhi yao wamepita shule maalum katika kazi hiyo lakini pia wako ambao wanaifanya kazi hii kwa uzoefu na mapenzi tu.
Naomba nikutoe hofu kuwa hata kama hujapita shule, ukiizigatia kwa makini makala hii basi utakuwa mwandishi mzuri.
Nawewe ambaye unatamani kuongeza ujuzi katika taaluma yako ya uandishi huna haja ya kuwa na wasi wasi. Nimekuandalia "njia 5 bora za uandishi wa makala bora.
Njia hizi ziko katika mtiririko maalum na ni lazima ufuatwe kama ambavyo nimeuweka hapa chini.....
TWENDE PAMOJA NAMI
Muandaaji ni mimi
- CHAGUA MADA (TOPIC)
- KICHWA CHA HABARI (HEADING)
- ANDIKA CHAPISHO / MAKALA YAKO
- TUMIA PICHA
- UHARIRI (EDITION)
Baada ya kuona mambo hayo matano hapo juu, sasa shuka chini kuona ni jinsi gani unaweza kukitendea haki kila kimoja hapo.
Nikukumbushe tu kuwa maoni yako kwetu ni ya thamani sana, hivyo ni vema baada ya kumaliza kusoma makala hii, shuka chini sehemu ya COMMENT na utuandikie, nasi tutayapata moja kwa moja.
1. CHAGUA MADA (TOPIC)
Hapa ndipo ambapo somo letu linaanzia.
Kwanza jiulize maswali haya muhimu;-
Je unataka kuzungumzia nini?
Je ambacho unataka kukizungumzia kinapendwa kiasi gani na wasomaji wako?
Je una elimu kiasi gani ya jambo ambalo unataka kulizungumzia?
Je ukiandika itakuwa na msaada wowote kwa wasomaji?
Kuelimika, kujifunza, kuburudika, kuhuzunika au kufurahi na kucheka ni mambo ambayo yanatakiwa walau moja lisikosekane katika andiko lako
Baada ya kupata majibu ya maswali hayo sasa unaweza kuchagua mada ambayo unataka kuizungumzia. Kama ambavyo mimi nimeamua leo kukuhabarisha juu ya "Njia za kuandika chapisho bora la Blog".
Ni matumaini yangu kuwa kuna kitu utakipata kutoka kwangu.
Lakini pia ukisha pata jambo ambalo unataka kulizungumzia, fanya yafuatayo.
- Chagua mada inayokuvutia
"NDIO" Narudia tena kwa harufi kubwa "CHAGUA MADA INAYOKUVUTIA WEWE"
Unaweza kuona kama nimekupiga chenga ya mwili lakini hapana.
Unajua kwanini?
Umewahi kuhamasishwa na mtu kupenda kitu? Kama jibu ni ndio basi ujue kuna asilimia kubwa mtu huyo aliyekushawishi kitu hicho yeye anakipenda.
Hivyo kama mada fulani inakuvutia wewe mwandishi ni rahisi kumuelezea mwingine naye akaifahamu kwa kina na akaipenda.
Hii ni kwa sababu kama kitu una kipenda ni rahisi kukifanyia uchunguzi wa kutosha na kuandika kwa ufasaha zaidi.
Kwakua mimi napenda sana uandishi, nataraji nami kukushawishi katika sanaa hii nawe uipende na kuona matunda yake.
Lakini huenda unachotaka kuandika kinapendwa sana na wengine basi jipendekeze kwa kitu hicho kwa wakati huo.
- Fanya uchunguzi (Research)
Soma, Uliza, Tafakari kisha andika kwa ajili ya wasomaji wako.
Lakini hata katika mambo ambayo unayafahamu vizuri ni vema ukayapitia kwanza kwa kina kabla ya kuyafikisha kwa hadhira.
Tunakuhakikishia kuwa nasi tumefanya uchunguzi wa kutosha juu ya hili. Hivyo usiwe na wasi wasi.
- Andika point muhimu (pembeni)
Wenye elimu zao walisema kuwa
"Kilichonakiliwa huhifadhiwa, na kilichokaririwa hupotea"
Maana ya kauli hii ni kwamba, unaweza ukawa umepata wazo la kuandika mada fulani na kupata point muhimu.
Basi usipoteze muda ziandike pembeni na uzihifadhi.
Jambo hili ni muhimu na ni bora ulifanye mara tu baada ya kupata wazo la kuandika makala yako.
Kuna muda unaweza kupata hamu ya kuandika jambo fulani kwa ajili ya wasomaji wako. Basi usiupuuze wakati ule kwani baadaye hamu inaweza ikatoweka na usiandike tena kwa ubora.
Andika (point) zako muhimu pembeni kwenye notebook au sehemu yoyote ambayo unaweza kuja kuichapisha baadaye.
2. KICHWA CHA HABARI
Hapa ndipo hasa Uchawi wa uandishi ulipo.
Wakati mwingine unaweza ukawa umeandaa makala nzuri na ya kufundisha sana lakini kichwa cha habari kikashindwa kumshawishi msomaji kusoma chapisho lako.
Kichwa cha habari lazima kizingatie mambo haya
- Kiwe na uwezo wa kumvuta mtu kusoma habari
- Kiwe kifupi (Ikiwezekana)
- Kiendane na mada husika
- Chepesi kusomeka na kueleweka
Mfano wa habari
Siku moja Jordan alisafiri kutoka Mwanza kwenda Mafinga. Alipofika kule hakuwakuta wenyeji wake kwani nao walisafiri kuelekea Mbeya jana yake.
Jordan hakuwa na simu lakini kibaya zaidi hakuwa na mwenyeji mwingine wala pesa ya matumizi.
Jordan aliamua kwenda mtaani na kuomba msaada kwa wananchi. Wananchi hawakumuamini kumpa pesa kwa kudhani kuwa alikuwa mwizi.
Usiku ulipofika, Jordan aliamua kujilaza mtaroni lakini kwa bahati mbaya polisi walimkamata wakidhani kuwa ni kibaka.
Swali je kichwa gani cha habari kinafaa katika habari hii? Chagua herufi ya jibu sahihi.
A. SAFARI YA JORDAN YA MAFINGA ALIYOTESEKA SANA KWAKWELI
B. MIKOSI UGENINI
C. KIJANA ALIYELALA NA NJAA BILA KULA MCHANA KUTWA
Jibu lako niwekee hapo chini katika sehemu ya COMMENTS
Nami ili nisikuchoshe
Kwa leo nitaishia hapa na usikose sehemu ya pili ambayo tutakufafanulia mambo matatu muhimu yaliyobakia katika mbinu 5 za uandishi wa makala bora.
Ahsante sana.
Ususahau kuja kutunuza namna ya kuifanya makala yako kuonekana google kwa urahisi
ReplyDeletePanapo majaaliwa mapema kabisa tutaweka hapa
DeleteNawashukru xana kwa msaada wenu
ReplyDeleteAsante sana kwa kuwa nasi.
DeleteB
ReplyDelete