Katika kipengele cha Afya leo tutagusa kuhusiana na ugonjwa KIFUA KIKUU / TB. Huenda umeshawahi kuusikia ama kuugua kama sio kumuuguza mwin...
Katika kipengele cha Afya leo tutagusa kuhusiana na ugonjwa KIFUA KIKUU / TB. Huenda umeshawahi kuusikia ama kuugua kama sio kumuuguza mwingine.

Hivyo nikaona ipo haja kukudokeza japo kwa uchache dondoo za gonjwa hili.
KIFUA KIKUU
Ni ugonjwa ambao husababishwa na bakteria wanaojulikana kama Mycrobacteria tuberculosis
Virusi hivi vipo katika aina tofauti kama vile
Mycrobacteria tuberculosis - Husababisha Kifua kikuu, mycrobacteria leprae - Husababisha ugonjwa wa ukoma na mycrobacteria bovis - Huathiri ng'ombe na binadamu
Ugonjwa wa kifua kikuu ni miongoni mwa magonjwa matatu ambayo hutokea sana kwa masikini duniani (Disease of poverty). Magonjwa mengine ni UKIMWI na MALARIA.
Kifua kikuu huathiri kwa asilimia 98
Ukimwi huathiri kwa asilimia 95
Malaria huathiri kwa asilimia 90
KUNA AINA 3 ZA KIFUA KIKUU
1. Active tuberculosis
Hiki ni kifua kikuu kinachosababisha madhara, hutokea pale ambapo bakreria waliopo mwilini wapo hai na wakati huo kinga ya mwili imeshindwa kuwadhibiti na hatimaye kusababisha madhara.
Mtu huyu anaweza kumuambukiza yeyote kwa njia ya hewa au majimaji kama vile kupiga chafya, kutema makohozi n.k
Pitia makala hii
2. Inactive tuberculosis
Hiki ni kifua kikuu ambacho hakiwezi kusababisha madhara kwa mtu mwingine, kwa kitaalamu aina hii hujulikana kama LATENT TB.
Hapa ni kwamba kinga ya mwili ya muhusika imeweza kuwazuwia bakteria kuweza kumuambukiza mtu mwingine. Mtu mwenye Latent TB huwa mara nyingi haoneshi dalili na wala hajiskii kuumwa.
3. Milliary tuberculosis
Huu ni ugonjwa uliosambaa mwilini na hutokea pale ambapo kinga ya mwili imepungua na kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu na kuenea kupitia damu na sehemu nyingine za mwili kama vile mishipa ya fahamu, mifupa, kibofu cha mkojo, ngozi, mfumo wa uzazi, viungo vya uzazi n.k
Ambapo husababisha homa, kupuungua hamu ya kula na kupunguza uzito.
DALILI ZA KIFUA KIKUU
- Maumivu makali ya kichwa
- Kupumua kwa shida
- Maumivu ya kifua
Ugonjwa huu huathiri sehemu ya juu ya mapafu na kusababisha kikohozi cha kawaida ambacho baadaye huweza kuongezeka na kuwa kikohozi cha damu au makohozi mazito. Lakini pia homa pamoja na kukosa hamu ya kula sambamba na kutokwa jasho jingi.
Dalili nyingine ni pamoja na;-
VIHATARISHI VYA KIFUA KIKUU
Watu hawa wapo hatarini zaidi kupata maambukizi ya Kifua kikuu
- Uzee (Wazee)
- Magonjwa yanayoathiri kinga ya mwili kama kisukari
- Wagonjwa wa Ukimwi
- Umasikini (Hali duni ya maisha)
- Unywaji pombe kupitiliza
- Kuishi sehemu zenye mlundikano mkubwa wa watu
- Utapia mlo
- Baadhi ya dawa za maumivu ya mifupa (athritis)
- Wahudumu wa afya
Pita na hapa
TIBA
Tiba ya kifua kikuu ipo, ni dawa ambazo mgonjwa atatumia kwa muda wa miezi sita mpaka tisa. Kwa miezi miwili ya kwanza mgonjwa atatumia dawa ya Rifampicin na pyrazinamide na miezi minne atatumia Isioniazid, Rifampicin na ethambutol.
KUJIKINGA NA KIFUA KIKUU
- Ziba pua na mdomo wakati wa kupiga chafya

Makala hii ni muhimu kwako
Mazoezi ya mara kwa mara ili kuimarisha kinga ya mwili
Kuishi katika nyumba yenye mfumo mzuri wa kuingiza hewa. Iwe na madirisha na milango mikubwa
Kutumia dawa maalum ya Isoniazid kwa wenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa huu
Kupata usingizi wa kutosha
Chanjo ya Kifua kikuu ipo na inafanya kazi na imesaidia watu wengi
Imarisha kinga ya mwili kwa kula vyakula vyenye virutubisho muhimu kwa afya bora
Asante sana kwa kuwa nasi, unaweza kutuwekea maoni yako hapa chini juu ya hiki ambacho tumekifanya.
COMMENTS