
Lakini pia yako madaraja ambayo yamejengwa kwa ajili ya kuepuka misongamano ama manufaa mengine ya wanadamu.
Hapa nimekuletea orodha ya madaraja 10 marefu zaidi duniani. Madaraja haya nimeyachanganya kwa ujumla yaani yaliyojengwa juu ya maji, angani na vile vile njia za reli.
Muandaaji na Mwandishi ni Saidi Bunduki
10. MENCHAC SWAMP BRIDGE

09. WUHAN METRO BRIDGE

08. LAKE PONTCHAR TRAIN CAUSEWAY BRIDGE
Unaambiwaje? Hili ndilo daraja refu zaidi duniani katika madaraja ambayo yamepita chini ya maji. Hizi ni takwimu za mwaka 2011. Ila ukichukua madaraja yote kwa ujumla hili linashika nafasi ya 8 kama ilivyo hapa kwenye orodha hii.
Pitia na makala hii
FAHAMU KUHUSU MICHEZO MAARUFU YA GOOGLE DOODLE
Daraja hili lina urefu wa maili 23.83 sawa na kilomita 38 na lina LINE mbili zilizoachana. Daraja hili limekatiza katika ziwa Pontchartrain huko katika jimbo la Louisiana ya kusini nchini Marekani na lilijengwa mwaka 1969. Picha yake ni kama linavoonekana hapo chini.

07. BEIJING GRAND BRIDGE
Huu ni miongoni mwa miradi mikubwa ya reli ya mwendokasi nchini China ambayo huunganisha miji mikubwa ya Beijing na Shanghai. Daraja hili lilikamilika mwaka 2010 na urefu wake ni maili 29.92 sawa na kilomita 48.
Kielelezo cha chini kuonesha Daraja hilo.

06. BANG NA EXPRESS WAY

05: WEINAN WEIHE GRAND BRIDGE
Daraja hili lililoko katika miji ya Zhengzhou na Xi'an nchini CHINA lina urefu wa futi 261,000 ambazo ni sawa na kilomita 79.5

04: TIANJIN GRAND BRIDGE
Tianjin ni mji wa nne kwa ukubwa nchini CHINA ambao upo katika pwani kati ya mjia wa Beijing na Shanghai.
Daraja hili limepewa jina la mji huu na lilikamilika mnamo mwaka 2010 na kufunguliwa rasmi mwaka 2011. Urefu wake ni futi 373,000 ambazo nia sawa na kilomita 113.
Kwa hapa Tanzania huu ni zaidi ya Umbali wa kutoka Mbeya hadi Tunduma. Nimekuwekea picha yake hapa chini.

Pitia na makala hii
MIJI KUMI HATARI ZAIDI BARANI AFRIKA
03: CANGDE GRAND BRIDGE
Hili ni daraja ambalo limeshika nafasi ya tatu kwa urefu katika madaraja ya njia ya reli. Urefu wake ni futi 380,000 ambazo ni sawa na kilomita 115.
Daraja hili lilikamilika mwaka 2010 na linapatikana nchini China. Tunaomba radhi kwani Hatukufanikiwa kupata picha yake.
02: CHANGHUA - KAOSIUNG VIADUCT
Ni miongoni mwa madaraja ya reli ya treni za mwendokasi huko Taiwan.

01: DANYAN - KUNSHAN GRAND BRIDGE
Dayan - kunshan Bridge lilikamilika ujenzi wake mnamo mwaka 2010 na kufunguliwa rasmi mwezi wa sita mwaka 2011. Daraja hili ni sehemu ya reli ya mwendo kasi ya Beijing kuelekea Shanghai nchini CHINA.
Fahamu pia
Urefu wake ni futi 540,000 ambazo ni sawa na kilomita 164. Na hili mpaka sasa ndilo hushikilia rekodi ya madaraja marefu zaidi Duniani (Kwa madaraja ya aina zote yaani nchi kavu, majini na relini) Picha yake ni hii hapa chini

Je ? una maoni / ushauri au mapendekezo?
Tuandikie hapo chini katika sehemu ya COMMENTS
Safi
ReplyDelete