Habari yako msomaji wangu mpendwa. Tuguse kidogo juu ya kuondoa sumu zilizopo katika miili yetu. Maradhi mengi yanasowasumbua watu hutoka...
Habari yako msomaji wangu mpendwa.
Tuguse kidogo juu ya kuondoa sumu zilizopo katika miili yetu.
Maradhi mengi yanasowasumbua watu hutokana na sumu zilizopo katika miili, mabadiliko ya hali ya hewa, mtindo wa maisha ni miongoni mwa sababu kubwa zinazosababisha sumu hizi.
Sumu hizi hutokana na vyakula, vinywaji bila kusahau mazingira tunayoishi na mabadiliko ya hali ya hewa.
TUNAPATAJE SUMU?
Zipo njia kadhaa ambazo ndizo hasa husababisha sumu katika miili yetu, lakini hapa nitakutajia njia kuu mbili.
1. HEWA
Ukweli ni kwamba hatuwezi kuishi bila kuvuta hewa ama sivyo? Lakini wakati mwingine tunavuta hewa ambayo imeshachafuliwa na kemikali mbali mbali kama vile kemikali na moshi wa viwandani, mashambani, moshi wa sigara n.k
Katika hali hii unaweza kujiona kuwa uko salama lakini kumbe tayari umeshapandikiza sumu katika mwili wako.
Je? sisemi ikiwa ndio mtindo wako maisha ya kila siku!! Hapo utagundua kuwa tunaishi na sumu nyingi mwilini
2. VYAKULA
Tunakula ili tuishi, lakini tukila chakula ambacho si sahihi maisha hayawezi kuwepo tena (tutakufa)
Hili limekuwa ni janga kubwa katika ulimwengu wetu wa sasa, vyakula vingi tunavyokula vimepitia viwandani na kuwekwa kemikali ambazo kwa asilimia kubwa ni sumu, bila kusahau vinywaji.
Sumu hili hutumaliza kidogo kidogo bila wenyewe kujua kwani unaweza kujihisi uko salama, au kuona dalili ndogo ndogo kama kuumwa na kichwa, tumbo, viungo na hatimaye kupuuza.
3. MADAWA
Utumiaji wa dawa kiholela ni tatizo kubwa katika kusababisha madhara badala ya kuponya. Kwa mfano mtu anaweza kupata maumivu ya kichwa, bila kwenda kwa wataalamu wa afya akachukua dawa fulani na kumeza. Baada ya muda unakuwa ndio mtindo wake wa maisha bila dawa fulani hawezi kuwa sawa. Bila kujua kumbe anajimaliza kidogo kidogo
Sasa tufanyeje kuepukana na hili?
SULUHISHO
Hapa nimekuandalia njia 7 ambazo zinaweza kuondoa sumu zilizolimbikizana mwilini mwako na kukufanya uepukane na magonjwa ya mara kwa mara
1. Fanya Mazoezi
Fanya mazoezi japo kwa nusu saa kwa kila siku, hakikisha umetoka jasho kwani jasho hutoa sumu mwilini. Kimbia, piga push up, ruka kamba, tembea kwa mguu walau kilomita 3 kila siku.
Huenda makala inayohusiana na mazoezi ilikupita. Bonyeza maandishi hapa chini kuisoma
2. Vyakula vya asili
Punguza / acha kula vyakula vya asili kama vile mihogo, ndizi, viazi na kadhalika. Baadhi ya vyakula ambavyo tunatakiwa kupunguza ulaji wake ni pamoja na piza, baga, chipsi na vinywaji vya viwandani.
Kunywa juis ya matunda ambayo umeitengeneza mwenyewe nyumbani kwako. Na ni vizuri zaidi kunywa juis ya tunda la aina moja kama vile parachichi, embe, chungwa, nanasi n.k
3. Maji mengi
Maji huondoa sumu ambazo tulizinywa ama kula katika vyakula. Kunywa maji huondoa sumu lakini kunywa maji mengi ni faida zaidi. Huenda hujafahamu jinsi gani unaweza kunywa maji mengi kila siku bila kuathiri shughuli zako za kila siku
Soma makala hii
MBINU 5 ZA KUKUFANYA UNYWE MAJI MENGI ZAIDI
4. Acha vilevi
Pombe ni miongoni mwa vinywaji ambavyo hutoka viwandani na vyenye kemikali nyingi. Lakini pia acha matumizi ya sigara na vinavyofanana. Nadhani hili liko wazi hakuna haja ya maelezo mengi.
5. Vuta hewa safi
Miongoni mwa visababishi vya sumu mwilini tuliona kuwa hewa chafu ni miongoni mwake. Hivyo hakikisha katika makazi yako unapata hewa safi, ishi kwenye nyumba yenye madirisha makubwa ambayo yanapitisha hewa kwa wingi.
6. Punguza matumizi ya plastiki
Kitu ambacho huenda hufahamu ni kwamba vyombo vya plastiki vimetengenezwa na malighafi zenye kemikali. Hivyo unapoweka chakula hasa kikiwa chamoto ni rahisi kuiyayusha kemikali hiyo na kupata madhara.
7. Tumia dawa kwa uangalifu
Ni vizuri kutumia dawa kwa maelekezo ya wataalamu wa afya, tuachane na mazoea ya kumeza dawa kila tupatapo maumivu. Dawa zinaweza kuwa sumu na kuhatarisha maisha yetu.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhgpX4ZMbRLRC8d4fOYg2svjiiU9NSfk4vzAPkCnqudigHvpkSLeypiysluJAshbTWB8y9D6R2Yj2vD_fwqwA3r_NW6ZMZWQwuhQbrGgA4IF1JbelOOhotJMNKbUFTJSnDl2dDI_9q5Vko/w553-h294/image.png)
8.Fanya masaji
Masaji husaidia kuufanya mtiririko wa damu kuzunguka kwa ufasaha. Damu inapotembea vizuri hukusanya sumbu ambazo zingejilimbikiza na kuzipeleka katika sehemu stahiki kama vile ini na figona hatimaye kutolewa nje kwa njia ya mkojo.
HITIMISHO
Kila mtu anahitaji kuishi kwa afya njema na furaha, kwahiyo haya ni baadhi ya machache ambayo yatakufanya kuishi kwa amani na afya njema kwa kuondoa sumu mwilini mwako.
Utafanya jambo la busara endapo utashea na mwingine makala hii kupitia katika mitandao ya kijamii hapo chini sambamba na kutuachia maoni yako sehemu ya COMMENT
COMMENTS