1. Alosema kikohozi, hakukosea kusema Kuhusu haya mapenzi, nimemeza si kutema Linanidondoka chozi, nashindwa kurudi nyuma Yanipasa kufunguka...
1. Alosema
kikohozi, hakukosea kusema
Kuhusu
haya mapenzi, nimemeza si kutema
Linanidondoka
chozi, nashindwa kurudi nyuma
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
2. Uvumilivu
ni kazi, Na umenipita wima
Nimeona
niwe wazi, pendo limenisakama
Kwa
kusi na kaskazi, meli kwako imezama
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
3. Akili
imeniganda, naomba usilaumu
Uwe
pete niwe chanda, isitiri yangu hamu
Kiukweli
NAKUPENDA, Naomba ulifahamu
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
4. Kimya kimeniathiri, niliogopa kusema
Ukweli hili nakiri, nabeba hii lawama
Nakupenda mwanamwari, tuliza wangu mtima
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
5. Nimeipenda rangiyo, umejaaliwa kweli
Midomo pua sikio, macho yako ya goroli
Tafadhali sema ndio, uwe wangu wa halali
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
6. Ewe binti fulani, Nielewe ndugu yangu
Neno langu la moyoni, Wewe ni wa ndoto yangu
Ila pia samahani, Kama hili kwako chungu
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
7. Niamini nisemacho, sitaki kukuchezea
Kwa mimi nipendacho, nami uje funga ndoa
Na chochote utakacho, kweli nakutimizia
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
8. Naomba wako uturi, mtoto unanukia
Nataka nikusitiri, uwe wangu malikia
Nitunzie hii siri, mashoga kuwaambia
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
9. Na kama nimekuudhi, msamaha nipatie
Vigezo sijavikidhi, usisite niambie
Wangu nakuomba radhi, Jibu zuri nipatie
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
10. Kumi beti ya tamati, kalamu nawachilia
Nakikunja kibusati, Shairi namalizia
Mebaki msamiati, Je? Utaniridhia
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza

1. Alosema
kikohozi, hakukosea kusema
Kuhusu
haya mapenzi, nimemeza si kutema
Linanidondoka
chozi, nashindwa kurudi nyuma
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
2. Uvumilivu
ni kazi, Na umenipita wima
Nimeona
niwe wazi, pendo limenisakama
Kwa
kusi na kaskazi, meli kwako imezama
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
3. Akili
imeniganda, naomba usilaumu
Uwe
pete niwe chanda, isitiri yangu hamu
Kiukweli
NAKUPENDA, Naomba ulifahamu
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
4. Kimya kimeniathiri, niliogopa kusema
Ukweli hili nakiri, nabeba hii lawama
Nakupenda mwanamwari, tuliza wangu mtima
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
5. Nimeipenda rangiyo, umejaaliwa kweli
Midomo pua sikio, macho yako ya goroli
Tafadhali sema ndio, uwe wangu wa halali
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
6. Ewe binti fulani, Nielewe ndugu yangu
Neno langu la moyoni, Wewe ni wa ndoto yangu
Ila pia samahani, Kama hili kwako chungu
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
7. Niamini nisemacho, sitaki kukuchezea
Kwa mimi nipendacho, nami uje funga ndoa
Na chochote utakacho, kweli nakutimizia
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
8. Naomba wako uturi, mtoto unanukia
Nataka nikusitiri, uwe wangu malikia
Nitunzie hii siri, mashoga kuwaambia
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
9. Na kama nimekuudhi, msamaha nipatie
Vigezo sijavikidhi, usisite niambie
Wangu nakuomba radhi, Jibu zuri nipatie
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
10. Kumi beti ya tamati, kalamu nawachilia
Nakikunja kibusati, Shairi namalizia
Mebaki msamiati, Je? Utaniridhia
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza

COMMENTS